Mahakama yaitahadharisha Jamhuri kukwamisha usikilizwaji wa kesi ya Malisa na Boniface Jacob

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeitahadharisha Jamhuri kutokana na kukwamisha usikilizwaji wa awali wa kesi inayomkabili mfanyabiashara na mwanasiasa, Boniface Jacob na mwenzake, mwanaharakati Godlisten Malisa, ikisema inatoa ahirisho la mwisho.

Jacob, maarufu Boni Yai, mkazi wa Mbezi Msakuzi, Dar es Salaam na Malisa, mkazi wa Moshi, mkoani Kilimanjaro wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 11805/2024, wanadaiwa kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii, kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka wanadaiwa kutoa taarifa za uchochezi kuwa Jeshi la Polisi linaua raia, wakilihusisha na kifo cha mwananchi mmoja, Robert Mushi, maarufu Baba G.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo, ilipangwa leo Alhamisi Julai 4, 2024 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali, ambapo washtakiwa wangesomewa maelezo ya awali ya kesi.

Hata hivyo, imekwama kuendelea kutokana na upande wa mashtaka katika kesi hiyo kutokuwa tayari, hii ikiwa ni mara ya tatu inaahirishwa kwa sababu hizo.
 
Boni akipelekwa segere matata, kwa jinsi tyubu yake ilivyojaa, aki-pass wind, mahabusu hazitakalika, hasa ukizingatia anakula mayai ya kuchemsha
 
Back
Top Bottom