Mahakama ya Mwanzo Uyole yateketea kwa moto usiku huu

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
7,129
10,260
MAHAKAMA YATEKETEA KWA MOTO MBEYA USIKU HUU.

Mahakama ya Mwanzo Uyole jijini Mbeya imeungua kwa moto na kuteketeza kila kitu mahakamani humo ikiwemo taarifa na mafaili yote ya kesi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka mahakamani hapo tukio hilo limetokea usiku wa Mei 5 ambapo hadi kufikia majira ya saa tatu kila kitu katika mahakama hiyo kilikuwa kimeteketea.

Hata hivyo Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na wakazi wa Uyole ya kati ilipo mahakama hiyo wameshirikiana kuzima moto huo lakin jitihada hizo hazikufanikiwa.

Chanzo cha tukio hilo hakijafahamika mara moja lakini hakuna madhara yoyote ya kibinadamu yaliyotokea na viongozi mbalimbali wa serikali ya mtaa na kata wamefika eneo hilo na kuwashukuru wananchi walivyoshirikiana na jeshi la zimamoto kuzima moto huo licha ya kwamba mahakama na kumbukumbu zote kuteketea kwa moto huo..
IMG-20180506-WA0002.jpg
IMG-20180506-WA0001.jpg
IMG-20180506-WA0000.jpg
 
Yajayo yataendelea kutushangaza na kutuhuzunisha. Tanzania yetu imevurugwa na wahuni na wadhalimu.
 
Mmmh!!,kwa jinsi niijuavyo mbeya usikute hiyo ndiyo njia mbadala ya kuyalipa Maandamano ya Dada wa Taifa Mange yale yaliyodhibitiwa april 26.
 
Back
Top Bottom