Mahakama ya kadhi: Uhitaji wake na hali ilivyo Tanzania

albuluushiy

JF-Expert Member
Oct 2, 2013
1,404
686
(Ni busara sana kusoma hapa na kuelewa, ili kama taifa, tusigawanyike)

Mfumo wetu wa Sheria umejengwa kushughulikia mashauri ya kimila na Kiislamu. Mjadala huu unaweza kufanikiwa iwapo tutaweka mbele kujifunza na kutafuta maarifa kama ambavyo imani zote zinavyohubiri.

Tujadiliane kwa hoja na sababu huku mioyoni mwetu tukiwa na uelewa wa pamoja wa misingi inayotuleta pamoja kama Taifa, tukikusudia kujenga mwafaka na kufanya maridhiano. Tukiendelea na ile dhambi ya watakacho wengi dhidi ya wachache bila hoja na sababu kwa hakika itatutafuna na baadhi yetu tutasimama ili kuhukumiwa kiimani, kisheria na kihistoria leo na katika vizazi vijavyo.

Utangulizi

Suala la Mahakama ya Kadhi limekuwa mojawapo ya hoja muhimu sana hapa Tanzania, mjadala wake umechukua zaidi ya muongo mmoja. Ili kulielewa suala hili ni muhimu kujifunza kwa kiasi mfumo wa utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano na kisha kwa kiasi kuelewa ni wakati gani na kwa mazingira gani Mahakama za Kadhi huwepo. Sambamba na kuelewa mfumo wa utoaji haki ni vema pia kuelewa matumizi ya Sheria za Kiislamu au "Sharia law" kwa ujumla wake au kwa sehemu.

"Sharia Law" kwa ujumla wake ni pana sana na inajumuisha vitu vingi, uzoefu unaonyesha maeneo tofauti tofauti katika ngazi ya nchi wanatumia Sharia Law kulingana na mazingira pamoja na mahitaji ya eneo na jamii husika.

Matumizi ya Sharia Law kwa namna moja au nyingine yanategemeana sana na asili na historia ya eneo au jamii husika, eneo au jamii yenye Waislamu wengi kuliko waumini wa dini nyingine inawezekana Sheria Law ikatumika kwa ujumla wake. Maeneo ambayo idadi ya waumini wa dini ya Kiislamu inakaribia kulingana na waumini wa dini nyingine matumizi ya Sharia Law ni tofauti, na mara nyingi Sharia Law huwa inatumika kwa sehemu na hasa katika kutoa uamuzi katika mashauri yahusuyo ndoa, mirathi, talaka na wake.

Hata hivyo yako mazingira ambayo eneo au jamii fulani inaweza kuwa na waislamu wachache na Sheria Law ikatumika kwa sehemu. Mahakama ya Kadhi huwa ni chombo kinachopewa dhamana ya kutoa maamuzi juu ya mashauri yanayohusu waumini wa dini ya Kiislamu. Uhitaji wake, uanzishwaji, muundo na mfumo wake wa kiutendaji hutegemea mazingira ya jamii husika. Mazingira haya hutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine lakini msingi huwa ni historia, mfumo wa kisheria na idadi ya watu na uwiano wa waumini wa dini ya Kiislamu na dini nyingine.

Uwepo wa Mahakama za Kadhi pale ambapo Waislamu ni wengi kuliko waumini wa dini nyingine namna ya uanzishwaji wake pamoja na muundo wake huwa ni tofauti na katika mazingira ambayo Waislamu wana idadi sawa na waumini wengine na vivyo hivyo pale ambapo Waislamu ni wachache katika jamii husika.

Nitatumia mifano mitatu ya maeneo ambayo kuna matumizi ya Sheria Law (matumizi ya jumla au kwa sehemu) pamoja na uwepo wa Mahakama za Kadhi.

Mfumo wa utoaji haki Tanzania Bara

Kama nilivyoeleza hapo awali uwepo au kutokuwepo Mahakama ya Kadhi kimuundo na kiutendaji ndani kikatiba na katika sheria za nchi inategemea na mfumo wa kisheria au legal system katika eneo husika. Mfumo wa kisheria huwa unataarifiwa na historia, desturi, utamaduni na uhalisia.

Kwa hapa Tanzania mfumo wa sheria unataarifiwa na vyanzo kadhaa vya sheria au kwa Kiingereza huitwa "sources of law". Sheria ya Judicature and Application of Laws Act CAP 358 inatamka bayana kwamba vyanzo vya sheria ni pamoja na Sheria za Kurithi (baadhi ya sheria za Uingereza), Sheria za Kimila (Customary Laws), Sheria za Kiislamu (Islamic Laws), Statutory Laws (Sheria zinazotungwa na Bunge), Case Laws (Maamuzi yanayofanywa na Mahakama), Baadhi ya Sheria za Kihindi (Indian Acts) pamoja na Katiba ambayo ndiyo sheria mama.

Kwa maelezo tajwa hapo juu utagundua, mfumo wa sheria wa Tanzania Bara unajumuisha matumizi ya Sheria za Kiislamu katika muundo wake wa kimahakama kuanzia Mahakama za Mwanzo. Kifungu cha 11(1)(ii) kinaweka bayana masuala ambayo kidesturi katika maeneo mengine yangekuwa chini ya Mahakama ya Kadhi kwamba yanaweza kuamuliwa na mfumo wetu wa kimahakama, kama kinavyojieleza "nothing in this subsection shall preclude any court from applying the rules of Islamic law in matters of marriage, divorce, guardianship, inheritance, wakf and similar matters in relation to members of a community which follows that law".

Kifungu hiki kinamaanisha "Mahakama yoyote haitazuiwa kutumia kanuni za Sheria ya Kiislamu katika masuala ya ndoa, talaka, malezi, urithi, wakf na masuala yahusianayo kwa waumini wa dini ya Kiislamu", tafsiri ni yangu.

Katika kuonyesha kwamba mfumo wetu wa kisheria tangu awali umekuwa na dhamira ya kuona masuala ya Waislamu na watu wafuatao mila (customs) yanafanyiwa maamuzi na mifumo na taasisi zetu zenye dhamana ya kutoa haki nchini utagundua hata Sheria ya Magistrate and Courts Act CAP 11 katika kifungu chake cha 7(3) inasema; "In any proceeding in any other magistrates' court in which any rule of customary or Islamic law is in issue or relevant the court may, and when directed by an appropriate judicial authority shall, sit with an assessor or assessors; and every such assessor shall be required, before judgment, to give his opinion as to all questions relating to customary or Islamic law in issue in, or relevant to, the proceeding; save that in determining the proceeding the court shall not be bound to conform with the opinion of the assessors".

Sheria hii inaendelea kutoa mamlaka kwa mfumo wetu wa kimahakama kutoa uamuzi juu ya Mashauri yanayohusu waumini wa dini ya kiislamu na hata wasio waislamu kisheria. Sheria inaweka bayana kwamba wakati shauri la kimila au kiislamu linapoletwa katika mahakama za mwanzo, hakimu atakaa na washauri ambao wataipa ushauri mahakama katika suala husika.

Washauri hawa wanapaswa wawe wamebobea katika eneo husika. Sheria inakwenda mbali zaidi kuweka vigezo vya aina ya washauri na namna ya kupatikana kwao ikiwemo hata marupurupu yao, rejea kifungu cha 9 cha Sheria (MCA CAP 11).

Aina za utolewaji haki kwa masuala ya Kiislamu

Suala la utolewaji haki katika mashauri ya Kiislamu hasa yale yahusuyo ndoa, talaka, malezi, urithi, wakf na masuala yahusianayo kwa waumini wa dini ya Kiislamu ni masuala ya kitaaluma, ni masuala ya elimu, "ilmu" au kwa Kiingereza ningesema ni jurisprudential na kwa kiasi fulani tofauti na imani na dini nyingine.

Nifafanue aina mbili za Mahakama za Kadhi na kama ambavyo zilivyo Zanzibar na katika nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Nigeria, India n.k.

Ziko Mahakama za Kadhi zenye mrengo wa Ibada au kwa lugha nyingine "Ibadat", Mahakama hizi na utendaji wa shughuli zake husimamiwa na taasisi za kidini na ni sehemu ya ibada. Mfano wa Mahakama za Kadhi zenye mrengo wa "Ibadat" ni katika baadhi ya majimbo ya kaskazini kule nchini Nigeria.

Mara nyingi hutumia sharia law kwa ujumla wake. Wenye dhamana ya kuamua mashauri katika mahakama hizi huwa ni viongozi wa kiimani wenye uelewa na sharia law. Mahakama zenye mrengo wa ibadat huwa huru "independent" na maamuzi yake huwa ya mwisho na kikatiba huwa si sehemu ya Mamlaka ya Dola hasa pale inapokuwa dola linaundwa na waumini wa dini mbalimbali.

Uko utaratibu wa kutoa haki kwa masuala ya Kiislamu kwa misingi ya elimu ya dini au kwa lugha nyingine "Muamalat", utaratibu huu umejikita katika taaluma ya sheria za Kiislamu kwa maana ya matumizi, maamuzi na watoa maamuzi kwa maneno mengine misingi yake imejengwa zaidi katika uelewa na maarifa ya taaluma ya sheria au jurisprudence. Wanaotoa maamuzi si lazima wawe viongozi wa kiimani pekee bali wale waliobobea katika sheria za Kiislamu au Islamic law.

Utolewaji haki kwa mashauri ya Kiislamu katika msingi wa Muamalat katika maeneo na nchi tofauti tofauti na kulingana na historia, mapokeo, uhalisia wa mfumo wa kisheria pamoja na mtangamano wa watu kutoka dini mbalimbali zinachukua sura kadhaa wa kadhaa, moja, msingi mkuu si ibada bali taaluma ya sheria, pili, katika baadhi ya maeneo utaratibu huu ni sehemu ya mfumo wa kisheria na kitaasisi na sehemu ya Mamlaka, mfano mzuri ni Zanzibar.

Tatu, katika maeneo mengine na nchi kadhaa utolewaji haki kwa masuala ya Kiislamu ni sehemu ya mfumo wa sheria unaoelekeza namna ya utolewaji haki katika mashauri ya Kiislamu na mfano mzuri ni katika baadhi ya majimbo ya kusini mwa Nigeria na hapa Tanzania Bara, kabla na baada ya uhuru.

Mfano wa hakimu (mwajiriwa wa Serikali) aliyefanya kazi kabla ya uhuru akitoa hukumu kwa mashauri ya Kiislamu wa weledi mkubwa ni Mathiasi Mnyapala aliyekuwa Liwali hapa Dar es Salaam. Miaka ya themanini Mwishoni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilipeleka wanafunzi wawili kwenda kusomea shahada ya uzamili katika Sheria za Kiislamu katika Chuo Kikuu cha London SOAS ambao leo hii ni Jaji Profesa Ibrahim Juma, Jaji wa Mahakama ya Rufaa na Jaji wa Mahakama Kuu Robert Makaramba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Biashara. Tujifunze kwa wanataaluma hawa.
Je, ni Ibadat au Muamalat?

Hitaji la Mahakama ya Kadhi linapaswa kuenda sambamba na swali la ni Je, ni utaratibu upi wa kutoa haki kwa mashauri ya Kiislamu, ni "Ibadat" au "Muamalat"? Kama jibu ni Ibadat basi waumini wa dini ya Kiislamu wanapaswa kutoa uongozi katika hili, ibada ni suala la imani na ni budi kwa waumini kulifanyia kazi ili Mahakama zilizoanzishwa zikidhi hitaji. Sheria ya Ndoa au Law of Marriage Act CAP 29 ni mfano mdogo wa kuanza kutambua nafasi ya Kadhi katika ndoa kama sehemu ya Ibada.

Kama jibu ni Muamalat basi jibu ni kwamba Mfumo wa Kisheria wa Tanzania Bara tayari umejumuisha kama chanzo cha Sheria zake, Sheria za Kiislamu au Islamic Law. Kinachotakiwa kufanyika ni kufanyia kazi maelekezo ya Sheria ya The Islamic law (Restatement) Act CAP 375 katika kifungu chake cha 2 na 3. Nimefuatilia jambo hili na ninashauri waumini wa dini ya Kiislamu wakae na waziri wa Sheria walimalize hili ili Mahakama zetu ziweze kutoa hukumu kwa mashauri ya Kiislamu zikiwa na mwongozo sahihi.

Asanteni, tutazidi kuelimishana.

Chanzo: Goodluckies Good
 
Kadhi Court is unconstitutional and covers a certain group of people. In fact, we don't even know who will control said courts. There are Shia and Sunni among other Islamic denominations, now, will Sunnies be ready to stand before a Shia Judge?
 
Ndugu albulushiy umetoa somo zuri lenye maelezo ya kutosha kuhusu mahakama ya kadhi. Kwa bahati mbaya wale wasioitakia mema nchi hii wataendelea kupinga tu hata kama hawana hoja ya msingi. Na kwasababu ya chuki zao binafsi dhidi ya uislamu wataendele kuziba masikio yao.
 
Kadhi Court is unconstitutional and covers a certain group of people. In fact, we don't even know who will control said courts. There are Shia and Sunni among other Islamic denominations, now, will Sunnies be ready to stand before a Shia Judge?

Kwa kiswahili......BAKWATA na SHIA kuna uhusiano wowote...??mtazamo wako ... Bakwata ni chombo cha kiislamu kinachotambuliwa na serikali na Bakwata na Sunni...hapo vipi.........??
 
Kwa kiswahili......BAKWATA na SHIA kuna uhusiano wowote...??mtazamo wako ... Bakwata ni chombo cha kiislamu kinachotambuliwa na serikali na Bakwata na Sunni...hapo vipi.........??
Muhammadans needs to answer me.
 
Back
Top Bottom