Mahakama Kuu Tanzania yaamuru kusikilizwa upya kesi iliyokuwa inamkabili Mhasibu wa zamani wa TAKUKURU

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
51,737
61,281
Kigogo huyo alikuwa anashitakiwa Kwa kosa la kuwa na Mali ambazo Hazina maelezo karibia Bilioni 4.

Mahakama Kuu imemuachia huru lakini akatiwa mbaroni tena Kwa DPP kukata Rufaa.

My Take
Mwenye pesa hajawahi fungwa hapa Tanzania labda Gen-Z waje wajitoe ufahamu ndio heshima itakuja.

====

1719650326647.png

Mahakama Kuu Tanzania, imeamuru kusikilizwa upya kesi iliyokuwa ikimkabili mhasibu wa zamani wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Geofrey Gugai na wenzake watatu, ambao walishinda kesi na kuachiliwa huru Novemba 2021.

Katika kesi hiyo, Gugai pekee alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuwa na mali zisizo na maelezo, zenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.63.

Hukumu ya kusikilizwa upya kwa kesi hiyo imetolewa jana Juni 28, 2024 na Jaji Musa Pomo wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) dhidi ya Gugai na wenzake.
 
"...Tatizo mnakula sana... ukila sana utavimbiwa... kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake..." Alisikika kiongozi wao
Ukizidisha kamba hayo ndio matokeo.Kila mbuzi hula Kwa urefu wa kamba yake, Kiongozi Yuko Sahihi au wewe unaona kuna shida?
 

Attachments

  • VID-20240629-WA0008.mp4
    2.8 MB
Back
Top Bottom