MahedeMkorofi
Member
- Jul 12, 2016
- 74
- 123
Kwa taarifa nilizopata kutoka kwa viongozi wa CHASO na BAVICHA Dodoma ni kwamba yale mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu vya Dodoma ambayo yalishindwa kufanyika baada ya kuzuiliwa na polisi, sasa yatafanyika tarehe 23 july.
Mahafali hayo yanafanyika baada ya Polisi kutoa ufafanuzi ya kwamba hawajazuia matukio ya ndani ya kisiasa.
Tulipotaka ufafanuzi juu ya kwanini waliamua kufanya mahafali hayo siku ambayo CCM watakuwa wanafanya mkutano mkuu wao, walidai ya kwamba ni siku ambayo wanachuo wote watakuwa huru baada ya mitihani yao, pia hawaoni tatizo sababu mahafali yao yanafanyika katika ukumbi tofauti na ule wa CCM. Pia walidai ya kwamba tayari wameshapata kibali cha kufanya tukio hilo na wamehakikishiwa ulinzi wa kutosha, hivyo wanawaomba watu wanaopenda kuhudhuria tukio hilo kuwa na amani.
Mgeni rasmi siku hiyo anatarajiwa kuwa mjumbe wa kamati kuu na aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa.