Mahafali hewa za kisiasa za wanavyuo ambao hawajamaliza vyuo zipigwe marufuku

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Kisheria mahafali za vyuo ni zile zinazofanywa na vyuo vyenyewe.Sasa hivi kumeibuka ufanyaji mahafali hewa za kisiasa za wanafunzi wa vyama vya siasa kufanya kile kinachoitwa mahafali ya kumaliza vyuo kwa milengo ya kisiasa.

Unakuta yanayoongelewa hayana hata na uhusiano na mahafali na wala hivyo vyama vinavyofanya hayo mahafali hewa hata shule ya chekechea hawana.Wanataka tu kutumia mahafali hayo hewa kufikia tu malengo ya kisiasa.

Mtu eti unampa cheti cha kumaliza chuo ambacho hajamaliza hata mitihani ya mwisho hajafanya.

Vyuo wafelisheni wote wanaofanya mahafali hizo za kisiasa video CLIP zipo mwaweza waona wote.Wafelisheni wanadhalilishaji mahafali za vyuo.

Kwa nyerere ilikuwa ukifanya sherehe kabla ya uteuzi akijua hakupi.Hawa nao wanafanya walimu wao hawana akili kuwa watake wasitake wao wameshafaulu na wanafanya sherehe ya mahafali kabla ya mitihani ya mwisho.Ni dhihaka kwa maprofesa
 
inaoneka wewe huna Elimu ya juu.

swissme
 
Ile ya ccm jana Uringa na ile ya dsm wiki mbili zilizopita mgeni rasm akiwa Jk ndio zilizokuwa hewa tena za vilaza...
 
....

....ujima bado upo na evolution bado inaendelea ...wakifelishwa wewe na jamii yako mtapata faida gani???? ......homooludupai !!!!
 
Ulifika walau kidato cha nne??? Maafali ulishawahi kufanya??? Ilikuwa baada ya kuhitimu au kabla ya kuhitimu.
Tulikuwa hatufanyi mahafali balli closing day ya kumaliza kidato cha nne iliyoshirikisha shule yenyewe,wazazi,wageni waalikwa na haikuwa ya kichama.Na ilifanyika shuleni.Ilikuwa haiitwi graduation day!!!!
 
hawa walilindwa na polisi ila UKAWA walipigwa na polisi , Tz ni yetu sote sio ya CCM tu
 
Za wa wapinzani si mmezivuruga..,? Kama ni video clip tuanze na za ccm zilizofanyika wiki mbili iliyopita dsm na iringa wafelishwe hao kwanza...unajitoa ufahamu kisa buku mbili???
Inaonekana wewe elimu yako ina walakini, kama una elimu ya juu hukustahili kuipata!!
 
YEHODAYO hili bandiko lako linaonyesha umezeeka sana mpaka akili imerudi kwenye utoto.
Actually ni hivyo, kama sio utakuwa na excuse moja tu; kwamba sehemu ambayo ubongo ulitakiwa ukae kwenye kichwa chako kimekaa kinyesi!
 
 
Mwanafunzi yeyote aliye mwaka wa mwisho wa masomo yake anastahili kufanyiwa mahafali. Hata kama anamaliza Dec, mahafali yanaweza kufanywa hata January.
 
Binadamu na akose hata maumbile yanayomtambulisha jinsi yake lakini asikose haya. Kukosa haya ni kukosa utambulisho wa ubinadamu wako. Tunakoenda siko jamani!
 
inawezekana una hoja. tatizo unaileta ili kulinda double standards za jeshi la polis kipindi hiki. hatudanganyiki....
 
Kukusaidia tu mtoa post mahafali ya makundi ni jambo la kawaida sana tena sio vyuoni tu bali hata secondary. Makundi kama wakatoliki, waislamu, walutheri, msalaba mwekundu, roots and shoots, na vyama mbali mbali huwa wanapanga tarehe zao za kuagana nje ya ile graduation yenyewe. Wala hakuna la ajabu hapo
 
Wewe ni mzalendo
Naunga mkono hoja!
 
inawezekana una hoja. tatizo unaileta ili kulinda double standards za jeshi la polis kipindi hiki. hatudanganyiki....

Vyuo ndio vyenye hati miliki ya Mahafali.Mtu huwezi ibuka tu uchochoroni unasema unafanya mahafali ya chuo fulani na mgeni wa heshima atakayekabidhi vyeti atakuwa kibaka fulani wa Richmond.
Mahafali gani hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…