Magufuli ndio anatoa 'Coup de grace' kwa CCM

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
'Coup de grace' ni kitendo au tukio la kumalizia au kuharibu moja kwa moja kitu kilichokuwa kinaendelea kuwa dhaifu kila uchao.

Ni kama kumuua kwa kumpiga risasi askari mwenzako aliyeumia sana katika mapambano ili kumpunguzia maumivi na mateso.

CCM ilikuwa inaumia, ilikuwa inateseka vibaya,ilishachoka kabisa kabla ya Serikali ya Magufuli.

CCM ilikuwa kakikundi fulani hivi ka vibaka, majangili, mafisadi na watu wasiojua utendaji wala ufanisi.

Ila hao ndio waliokuwa wana CCM na ndio iliyokuwa CCM yenyewe na ndivyo ilivyo hata leo hii.

Ni chama chenye saratani ambayo kwakweli hakuna namna ya kuiponyesha na ndio maana Magufuli ameamua kuwa heri tu huyu mgonjwa afe kuliko azidi kuweweseka.

Wana CCM wenyewe wamebaki mabubu wakipambana nyuma ya pazia.
Wamebaki wasiojiamini kwa hoja kiasi kwamba pamoja na wingi wao bungeni hawawezi kujenga wala kujibu hoja na hawataki kabisa watanzania wauone huu upungufu. Hawataki TBC irushe bunge.

Ni wapiganaji waoga, aina ya wale wanaovizia mtu usiku wampige rungu la kisogo.
Wanafanya mikutano ya kisiasa lakini hawataki wapinzani wafanye.

Huku kwenye mitandao ya jamii wameajiri kasuku wa kuwapigia debe japo kwa mkopo ili tu kujaribu kujisitiri.

Coup de grace ni wana CCM kuitana majipu.
~Ni bomoa bomoa ya nyumba za masikini.
~Ni vita na matajiri.
~Ni Magufuli kukwepa mkwamo wa kisiasa Zanzibar
~Ni kupambana na mabenki nchini.
~Ni kuwa na mahusiano mabovu na Mataifa makubwa, jumuiya za kimataifa.
~Ni kunyamazia ubaguzi wa watu weupe na weusi Zanzibar.

Kuna msemo unaosema 'nionyeshe marafiki zako na mimi ntakwambia wewe ni nani'.
Magufuli hana rafiki na hapendi watanzania tuwe na marafiki.

Ni hatari kuwa na rais ambaye hatabiriki na ndio maana naamini kuwa Magufuli anaisaidia CCM kupumzika mapema kwa kuiua.
 


Tafiti zako labda zitakubalika kwa Wanachadema wenzako tu lkn hakuna mtu mwenye akili Dunia hii anayeweza kukubalia kutokana na huu ukweli ufuatao; ukawa (Muungano wa vyama vyote) umepata Wabunge chini ya 80 wakati CCM imeshindwa Wabunge zaidi ya 200, Raisi wa JMTZ (CCM) amemshinda mpinzani wake wa ukawa kwa tofauti ya karibia asilimia 20 (20%) ya kura zote zilizopigwa hii ni tofauti kubwa sana kwa kiwango chochote kile kinachotumiwa na binadamu kwanza ingekuwa Vyama vya Kidemokrasia Viongozi wote wa ukawa walipaswa wajiuzulu kwani wameshindwa kabisa, chaguzi za Serikali za Mitaa ndiyo wala usiseme!

Kumbuka kwamba nimeongelea kuhusu ukawa na wala siyo chama kimoja kimoja, kama tukichukua kwa mfano chadema peke yake hali inakuwa mbaya zaidi!
 


Well said Mkuu!
CCM ndio inakatika roho kwa sasa! Na magufuli ndio mtoaji roho ya CCM.
 
Watuwengine akilizao zitakuwa zimekalia kwenye unyayo. Asa viongozi wa ukawa wajiuzuri kwa hoja ipi ya msingi? Ukiangalia trend ya kisiasa vyama vya upinzani vimepiga hatua tena kubwa sana. Maana tangu vyama vingi vianze ni mara ya kwanza msimuhuu kwa vyama vya upinzani kukamata halimashauri mojawapo ikiwa kinondoni. Mbona hatuwaambii hawa viongozi wetu wa ccm walio gawa halimashauri hizi kwa ukawa. Mm ni kada wa ccm ila nina mashaka juu uwezowako wa kufikiri unaposema viongozi ukawa wajiuzuri.
 
Huko kubebwa na tume ndo unaiita ushindi hata hiyo link kama sio chaguzi hii ccm imeongoza kwa 20% ya kubebwa na time,kama chama che demokrasia waliogopa nini Matokeo ya uchaguzi zenji kutangzwa acha kujitia ukichaaa
 
Huko kubebwa na tume ndo unaiita ushindi hata hiyo link kama sio chaguzi hii ccm imeongoza kwa 20% ya kubebwa na time,kama chama che demokrasia waliogopa nini Matokeo ya uchaguzi zenji kutangzwa acha kujitia ukichaaa


Sawa basi tuweke pembeni Uraisi ambao mnasema mmeibiwa ingawaje mpaka leo hii haman ushsidi wowote ule mliotoa zaidi ya maneno tu!

Vipi kuhusu Ubunge? Kwa maana matokeo ya Ubunge mnayakubali sasa mbona tofauti ni kubwa sana? Ni zaidi ya mara mbili ukawa Wabunge 78 CCM zaidi ya 200!!!

Hapo vipi utamshawishi nani Duniani akuelewe kwamba Chama kilichoshinda viti zaidi ya 200 dhidi ya chini ya 80 eti kinakufa??
!!!

Ni mtu mwenye akili ndogo tu anayeishi kwenye Dunia yake mwenyewe ambayo kiuhalisia haipo ndiyo anaweza kufikiri hivi!
 
Well said mkuu. Ccm inatapatapa kabla ya kukata roho. Hatuoni kinachofanyika kupunguza ugumu wa maisha bali maigizo tu ya kutufanya tuwapende.
 
Figisu zilikuwepo kwenye ubunge pia. Si unajua hawakubali kushindwa.
 
Kwa wenye akili unaowasema na wewe upo?
Kwani hao UKAWA kabla ya uchaguzi walikuwa na wabunge wangapi? Na mshindi wa urais kutoka CCM hizo kura alizopata na hizo asilimia zake ni zaidi ya asilimia ngapi ukilinganisha na asilimia alizopata mshindi wa kura za Urais wa CCM kwa uchaguzi wa mwaka 2010?
Ukinijibu kwa hayo naweza kukufikiria vinginevyo,lkn kwa sasa ibaki kuwa kweli kwamba ulikurupuka kumjibu jamaa bila kutumia akili!
Nawe ni mmoja wa vijana waliopewa kazi za kukinadi chama kwenye mitandao ya kijamii? Nawe umesahaulika??
 
Barbarosa nilijua utajibiwa na nnaamini umeridhika na majibu.
Kwanza nikulaumu sana wewe binafsi kwa kupigia debe ubaguzi wa rangi Zanzibar.

Barbarosa ni aibu kubwa na wehu tu kushabikia ubaguzi wa rangi na hivi ndivyo ilivyo CCM ~ chama cha kibaguzi.
Mara muitane Magamba, mara majipu...
Ok poa hiyo fanyeni kwa level yenu ya chama maana ndio tabia yenu.
Ila kwa level ya taifa mtuhurumie, pumzikeni na taifa litapona na huu ugonjwa wa ubaguzi.
 


Soma kwanza Mada iliyoletwa ndiyo uandike, mada imesema kwamba CCM ilikuwa imechoka kabisa na sasa kuelekea kufa, sasa Chama kilichochoka kwa akili ya kawaida hakiwezi kushinda Uchaguzi kwa tofauti ya asilimia 20 (20%) ya kura zote zilizopigwa na hapo hapo kushinda zaidi ya viti vya Ubunge 200 dhidi ya chini ya 80 ya Mpinzani wake, hakuna mtu yoyote yule mwenye akili Dunia hii anaweza kuamini huwo utafiti!

Utafiti wake ungekuwa na maana kama CCM ingeshinda kwa tofauti ya asilimia 1 - 5 % lkn siyo 20% au mpinzani wangekuwa na viti sawa vya Ubunge au pungufu labda viwili lkn siyo 200 kwa chini ya 80 halafu unasema mwenye viti 200 anakufa???
 
Barbarosa ungejibu maswali yangu ungeelewa nasema nini, pengine ungetafakari kama hoja ulizotoa ni sahihi.

Unaelewa nini mtu akisema umaarufu wa chama unashuka?
 
Barbarosa ungejibu maswali yangu ungeelewa nasema nini, pengine ungetafakari kama hoja ulizotoa ni sahihi.

Unaelewa nini mtu akisema umaarufu wa chama unashuka?


Hakuna mahali ambapo mleta mada aliposema kwamba Umaarufu wa Chama unashuka, angesema hivyo hiyo ingekuwa ni mada nyingine lkn yeye amesema CCM amesema CCM ilikuwa imeshachoka na kuumia kabisa sasa matokeo ya uchaguzi hayaashirii Chama alichokielezea kwamba kimechoka na kuumia kabisa!
 
JK ametengeneza marafiki wengi huko nje katika safari zaidi ya 400 alizosafiri, mbona umasikini upo pale pale!. Wazungu hao hao wanatishia vikwazo. Afadhali naiona ndani ya hiyo hiyo CCM kulinganisha na huko kwenye upinzani ambapo bado ni kubovu. Wana UKAWA wengi humu JF wanajenga hoja nyepesi kiasi ambacho mtu anajiuliza hivi hawa wangepewa hii nchi madudu makubwa kiasi gani yangejitokeza.
 
You are a true great thinker , congratulation .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…