Kuna watu ambao wanakwambia nchi hii inahitaji rais asiye mkali, yaani mpole atakayechekea mambo ya kipuuzi. Wanigeria pamoja na umaarufu na ukubwa wa Taifa lao bado wanamchukulia Rais wetu kama mwalimu wao katika suala la leadership, wanautumia utendaji wa rais wetu ndani ya siku 100, katika kumfikishia ujumbe mzito rais wao ili aweze kuibadilisha nchi yao. Katika wagombea wote waliotaka kuiongoza nchi katika awamu ya tano, hakuna hata mmoja anayefikia angalau robo tu ya uwezo wa JPM. Lakini maneno matakatifu yanatuambia kwamba nabii huwa hapendwi kwao.