Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,343
- 118,616
Naomba kuanza kwa kudeclare interest, japo mimi ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini sio mfuasi wa mwanasiasa yoyote, wa chama chochote, ila kuna baadhi ya viongozi nilikuwa nawakubali sana!, John Pombe Magufuli, hakuwa ni miongoni mwao, kwa sababu kadhaa wa kadhaa, moja ikiwa ni style yake ya utendaji wake kazi, sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo kwa kufanya vitendo bila kuchelewa ila pia bila kufuata sheria, taratibu na kanuni!, ambayo ni zimamoto style, akilisikia jambo, ni actions tuu!, hapapasi, wala kumung'unya maneno, kwakwe ni kazi tuu, in a dictatorial manner, japo wengi pia wanamkubali kwa utendaji wa aina hii ya kidikiteta kwa hoja kuwa Tanzania hapa tulipofika, tulimhitaji sana kiongozi wa type ya Magufuli Style ili alinyoosha nchi hii. Mifano michache ya utendaji huu ni lile sakata la kile kituo cha Mafuta kule Mwanza, sakata la samaki wa Magufuli, hata sakata la uuzwaji wa Nyumba za Serikali, yametekelezwa kwa full pupa nyumba zimeuzwa hadi line police huku watu wakishangilia, lakini mwisho wa siku, Tanzania kama nchi, we paid the price, na kuna nyingine tutaendelea kulipa, msije kushangaa tukinunua ndege, hazitathubutu kukanyaga nje ya Tanzania kwa sababu zitadakwa kufidia ile Meli ya Samaki wa Magufuli!.
Naomba kukiri wazi kuwa kwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo ninavyozidi kumkubali huyu jamaa, na ndivyo nazidi kumuona anavyoshabihiana na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kitendo cha Nyerere kutupatia uhuru, na ukombozi dhidi ya wakoloni kiasi kwamba tulimbatiza jina la Musa!, na kweli ikawa kama alivyo Musa, hakuweza kuwaingiza wana wa Israel kwenye ile nchi ya ahadi, aliishia njiani, ila Mungu akawaahidi wana Israel kuwaletea Mkombozi, Masiya, kuikamilisha ile kazi ya Musa!.
Jee inawezekana kwa Tanzania, Magufuli ndiye yule masiya wetu?, yaani hatimaye Mungu ametukumbuka?!, kuna uwezekano Magufuli ndio yule masiya aliyetumwa na Mungu, kuja kuikamilisha ile kazi ya Musa wetu, kutukomboa ukombozi wa pili na kutufikisha kwenye ile nchi ya ahadi?!.
Mfanano na utofauti kati ya Magufuli na Nyerere ni kama ifuatavyo (Compare and contrast)
Nyerere alikuwa Mkristu, Magufuli ni Mkristu!.
Nyerere alikuwa Mkatoliki, Magufuli ni Mkatoliki!.
Nyerere alisali kanisa la St.Peters, Magufuli anasali St. Peters.
Rais Nyerere akiwepo, Misa za Sikukuu ziliendeshewa St. Peters na Muadhama Laurian, Kardinali Rugambwa.
Rais Magufuli akiwepo, Misa za Sikukuu zinaendeshewa St. Peters na Muadhama Policarp, Kardinali Pengo.
Nyerere was hardily seen in public smiling with his wife, Mama Maria.
Magufuli is hardily been seen in public smiling with his wife, Mama Janet.
Nyerere was hiring very careful and firing without a blink.
Magufuli is hiring ali mradi and firing the kutumbua type.
Wote wawili, Magufuli na Nyerere ni wasanii wa ngoma za asili maana wote wawili ni wapiga ngoma!.
Nyerere aliendesha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoia.
Magufuli anairudisha Tanzania chini ya chama kimoia.
Nyerere alichukia rushwa, Magufuli anachukia rushwa.
Nyerere akikasirika, anasema hovyo hadi kutukana, Magufuli pia anasema ovyo ila hatukani.
Nyerere alipanga, kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma, Magufuli anahamia Dodoma.
Nyerere alipanga kujenga Stigler Gorge, Magufuli anajenga Stigler Gorge.
Tofauti kati ya Magufuli na Nyerere
Kanisani Nyerere alitengewa mabenchi matatu ya mbele yote peke yake na walinzi wake!, mbele bench lilikuwa tupu, katikati alikaa yeye na Mama Maria na walinzi wawili, nyuma walikaa walinzi watatu!.
Magufuli, anakaa na waumini kama muumini, amejichanganya na watu na kuwa ni mmoja wao, miongoni mwao!.
Nyerere hakuwahi hata kusimama kwenye kipaza sauti kusalimia kanisani, au kutajwa yupo. Magufuli anatajwa, na amesimama kutoa salamu za Noeli!.
Wakati wa Nyerere, hakuna kamera kuingia kanisani akiwepo na hakuna kupigwa picha kwenye Ibada, Magufuli ni sio tuu kamera zinaingizwa kwenye ibada, hivyo ku draw unnecessary diverting attention, bali kamera zinapishana hadi video zinabanana!, katika hali inayoonyesha media was tipped before.
Nyerere alikuwa akitoka wa mwisho, anakuta watu wamejipanga nje kumsalimia!. Magufuli ametoka wa kwanza, huko nje zikuweza kuwahi kuona ilikuwaje!.
Nyerere ni dikiteta wa Aina yake, na Magufuli ni dikiteta wa aina yake. Kwa Nyerere demokrasia haikushamiri. Watu walipiga kura na kivuli, kwa Magufuli, watu watapiga kura na maboya.
Nyerere alikabidhiwa nchi ya vyama vingi, akavifuta na kuigeuza nchi ya chama kimoja. Ali suppress demokrasia na freedom of speech. Alitawala kwa mkono wa chuma with draconian laws ikiwemo Presidential Preventive Detention Act, Newspapers Act ya 1976, Magufuli ni dikiteta, aliyekabidhiwa nchi ya vyama vingi, ana supress democracy kwa kurudisha nchi chini ya chama kimoja kwa repressive legislations and draconian laws, ikiwemo media services act ya 2016, draconian statistics act, draconian cyber law, etc.
Ila udikteta wote wa Nyerere na Magufuli ni udikiteta wa uzalendo unaofanywa kwa nia njema ya kujenga na kulisaidia taifa.
Hivyo inawezekana kiukweli kabisa, John Pombe Joseph Magufuli ni Musa mwingine kama Nyerere, Mungu ndie amemtuma kuja kuikamilisha kazi ya Nyerere aliyoiacha ya kutuingiza taifa letu la Tanzania kwenye ile nchi ya ahadi!, ila hala hala na yeye asije kuwa kama Musa, hakuingia kwenye nchi ya ahadi, Nyerere pia hakuingia, Jee Magufuli atatufikisha?, au Nate...time will tell!.
Tumpe ushirikiano wa kutosha Magufuli atuingize kwenye nchi ya ahadi!.
Happy Boxing Day!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
NB. Mwandishi ni Mkisto, Mkatoliki wa kanisa la St. Peters, Mkomunio wa St. Peters, Akatumikia St. Peters, Akapata Kipaimara St. Peters, Akafungia ndoa St. Peters, alisali na Nyerere hapo St. Peters, na sasa anasali na Magufuli St. Peters!.
Kuna tofauti kubwa mno kati ya Magufuli na Nyerere...
Nyerere alipenda Media...hata waandishi wa kizungu hakuwaogopa
Nyerere alikuwa anajua kiswahili vizuri sana..hadi mafumbo na vijembe vya watu wa pwani
na kucheza bao...
Nyerere alipenda sana umasikini....kiaina fulani
watu masikini walikuwa hata wanaenda kucheza nae bao Msasani na Ikulu pia..
Nyerere alikuwa na uelewa mkubwa wa siasa za dunia...na alipenda mikutano
Nyerere alikuwa na umakini fulani hivi..huwezi kusikia wizara ya walemavu..halafu tena wizara ya ustawi wa jamii nyingine..
Nyerere alikuwa mtoto wa chief...uongozi ulikuwepo damuni...
Nyerere aliijua siasa..alikuwa mwalimu wa siasa na fitina zake..uliza kina Fundikira,bibi Titi,
Nyerere alipenda kuwa busy na siasa za bara lote la Africa..alikuwa na passion na siasa za kimataifa
Nyerere aliitwa 'Mussa' kwa kumkejeli...sababu ya kuwa mbishi na kutosikiliza sana wengine..
aliitwa pia 'baba haambiliki'...
thanksMagufuli hapendi umasikini...ndie Rais wa Kwanza kusema 'nchi hii Tajiri' na kuponda misaada...
Magufuli siyo mjamaa.....ndo maana kasema wazi mashirika yasiyo na tija yapunguze wafanyakazi
Nyerere alikuwa mjamaa..bora shirika lipewe ruzuku kuliko kufukuza wafanyakazi
Magufuli licha ya kuwa sio mjamaa..vilevile sio bepari..na misimamo yake binafsi ya kiuchumi haiko clear..
Magufuli hapendi media..hata hotuba za mwisho wa mwezi za Mkapa na Kikwete kafuta
Magufuli lugha..hata kiswahili tu ni shida
Magufuli licha ya kuwa mkatoliki kama Nyerere...sio mkatoliki kindakindaki kama Nyerere..Magufuli
kashaenda kwa TB Joshua na Fernandes....Nyerere usingeweza kumkuta huko infact alibana imazi hizo
hakukuwa na uhuru huo kama wa sasa wa kuanzisha makanisa....
Rejea:
Kwa wale wageni humu jukwaani wanaodhani Magufuli nimeanza kumuandika
leo, wakausome uzi huu!. Sio wengi wanaojua Magufuli kaibukia wapi na kwa nini ni yeye!.
Aug 15, 2014 nilipandisha uzi huu, Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 Ni John Pombe Magufuli!,
Feb 6, 2015, nilitoa angalizo hili, Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015
Baada ya CCM kumpitisha Magufuli kuwa mgombea wake, Jul 12, 2015 nilipandisha uzi huu, Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Yaishe!.
Baada ya uchaguzi nilipandisha nyuzi hizi, Ushauri Wa Bure kwa ENL, Chadema na UKAWA, Tuyakubali Matokeo.
If you can't beat them, join them! Lets Join Them!.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ..
Jumapili Njema
Paskali