Magufuli hajatumbua jipu hata moja tangu aingie madarakani

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Mh. Magufuli hajawahi kutumbua jipu hata moja tangu aingie madarakani 2015, badala yake amekuwa akihangaika na vipele uchungu tu.

Majipu haswa ni:
CCM kama jipu Kuu lenye majipu tawi, ambayo ni:-
Escrow
Lugumi
Richmond Dowans
Meli Chakavu
Nyumba za umma
IPTL
Rada
Meremeta
Kagoda
Kiwira
EPA
NBC
Kuchakachua uchaguzi
Kuchakachua katiba ya wananchi
Kupuuza sheria kanuni na taratibu za nchi na Utumishi wa umma.
Kuhamisha fedha za umma kinyume na sheria kanuni na taratibu.

Nawasilisha
 
Jingalao, hii unasemaje! Naona umeona Richmond :copy and paste please not original post
Vimeo vya Mhe. Mkapa vilivyotajwa ni:
Mkapa anahusishwa na umiliki wa mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kupitia kampuni yake ya ANBEN anayomiliki na mkewe, Anna ikiwa miongoni mwa makampuni matano yaliyoingia ubia na kampuni ya TanPower Resources Company Limited.

Mkapa, kupitia TanPower Resources Limited, anahusishwa na dhamana ya serikali ya kupata mkopo wa Sh. 17.7 bilioni kutoka CRDB Bank kwa ajili ya kuendeleza mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira.
Kwanza, inadaiwa kuwa Mkapa alimiliki kampuni akiwa bado rais (ANBEN 1998) wa nchi na hivyo atakuwa alitumia nafasi yake kujinufaisha binafsi na kampuni yake.

Pili, kwa kuwa alikuwa bado madarakani na kwa kuwa uamuzi wa kuuza Kiwira ulifanyika ndani ya Baraza la Mawaziri aliloliongoza, basi uamuzi huo ulikuwa wa upendeleo kwa kampuni yake.

Tatu, hata waziri aliyejenga hoja mbele ya baraza la mawaziri, Daniel Yona ametokea kuwa mshirika katika umilikaji wa mgodi huo, jambo ambalo haliendani na utawala bora.

Nne, mkataba wa kampuni ya Mkapa kuuza umeme kwa Tanesco ulifungwa Mkapa akiwa madarakani (Septemba 2005), jambo linaloonyesha upendeleo kwa kampuni yake na utovu wa utawala bora.

Miaka mitatu iliyopita serikali iliahidi kuurudisha mgodi wa makaa ya mawe mikononi mwa serikali jambo ambalo halijafanyika mpaka sasa licha ya kwamba vijana wengi wanahitaji ajira ukiacha mahitaji ya nishati ya umeme nyanda za juu kusini.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanajaribu kuongazia hatua atakazozichukua Mhe. Magufuli katika kuviondoa vimeo vya Mhe. Mkapa ikiwemo kupitia upya mikataba ya ubinafsishaji ili kuvirudisha mikononi mwa wananchi viwanda walivyopewa wawekezaji feki waliovigeuza magofu.

Swali linakuja, je muda bado au ndo tusamehe na kusahau kuhusu vimeo hivyo?
 
Sibiria kivumbi mwezi wa saba mahamaka yenu [mafisadi] itakapoanzishwa...hapo ndo mtajua jamaa yuko serious au anabeep...
agopa sana mwanasiasa aliyechaguliwa na watu anayefanya mahamuzi magumu huku akisisitiza kuwa yeye kawekwa na Mungu
 
Jingalao, hii unasemaje! Naona umeona Richmond :copy and paste please not original post
Vimeo vya Mhe. Mkapa vilivyotajwa ni:
Mkapa anahusishwa na umiliki wa mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kupitia kampuni yake ya ANBEN anayomiliki na mkewe, Anna ikiwa miongoni mwa makampuni matano yaliyoingia ubia na kampuni ya TanPower Resources Company Limited.

Mkapa, kupitia TanPower Resources Limited, anahusishwa na dhamana ya serikali ya kupata mkopo wa Sh. 17.7 bilioni kutoka CRDB Bank kwa ajili ya kuendeleza mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira.
Kwanza, inadaiwa kuwa Mkapa alimiliki kampuni akiwa bado rais (ANBEN 1998) wa nchi na hivyo atakuwa alitumia nafasi yake kujinufaisha binafsi na kampuni yake.

Pili, kwa kuwa alikuwa bado madarakani na kwa kuwa uamuzi wa kuuza Kiwira ulifanyika ndani ya Baraza la Mawaziri aliloliongoza, basi uamuzi huo ulikuwa wa upendeleo kwa kampuni yake.

Tatu, hata waziri aliyejenga hoja mbele ya baraza la mawaziri, Daniel Yona ametokea kuwa mshirika katika umilikaji wa mgodi huo, jambo ambalo haliendani na utawala bora.

Nne, mkataba wa kampuni ya Mkapa kuuza umeme kwa Tanesco ulifungwa Mkapa akiwa madarakani (Septemba 2005), jambo linaloonyesha upendeleo kwa kampuni yake na utovu wa utawala bora.
Miaka mitatu iliyopita serikali iliahidi kuurudisha mgodi wa makaa ya mawe mikononi mwa serikali jambo ambalo halijafanyika mpaka sasa licha ya kwamba vijana wengi wanahitaji ajira ukiacha mahitaji ya nishati ya umeme nyanda za juu kusini.
Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanajaribu kuongazia hatua atakazozichukua Mhe. Magufuli katika kuviondoa vimeo vya Mhe. Mkapa ikiwemo kupitia upya mikataba ya ubinafsishaji ili kuvirudisha mikononi mwa wananchi viwanda walivyopewa wawekezaji feki waliovigeuza magofu.
Swali linakuja, je muda bado au ndo tusamehe na kusahau kuhusu vimeo hivyo?
Mimi nilikuwa naweka list sawa tu msije mkafuta kama kule kwenye website yenu...mleta mada aongezee na hiyo kashfa ya Richmond iliyosababisha Waziri mkuu kujiuzulu...!
 
Imeshaongezwa tayari. Richmond Dowans ni zao la CCM na mhusika halisi yupo CCM, na unamfahamu
 
Back
Top Bottom