CWT ni kikundi cha wajanja wajanja wachache wanaotafuna michango ya walimu. Mikoani na wilayani ni makatibu hawa ni waajiriwa na chama, kazi yao ni kuhakikisha wanachaguliwa wenyeviti wa wekahazina mbumbu ambao hawana uelewa wa kutosha. Niliona salary slip ya mwalimu mmoja rafiki yangu anachangia aslimia 2 ya mshahara wake kila mwezi anakatwa zaidi ya elfu 30. Kwa mwaka anakatwa zaidi ya laki 3. Mwalimu akiajiriwa tu serikali inaanza makato bila kujaza fomu ya kujiunga na chama hiki. Kila mwaka ikifika Mei mosi ya mwaka anapewa T shit na kofia isiyozidi elfu 10. Akisitaafu baada ya kuchangia miaka kama 30, zaidi ya miezi 360 sawa na sh 10,800,000 kama mshahara wake hautabadilika kwa kipindi chote cha utumishi wake atashikwa mkono kwa kupewa bati za sh. laki tatu. Serikali ikionesha kutaka kuwatete inatishwa na viongozi CWT kutaka kuhamasisha mgomo kwa walimu kwa kutetea madai yasiyoisha. Serikali inatulia, wajanja hawa wanaendelea kuwanyonya walimu wenzao.