Magufuli Aliposhangiliwa Kubana Matumizi

incorruptible

Member
Apr 19, 2014
62
46
Vituko vya Kubana Matumizi

Aliposema wanafuta safari za nje kuokoa hela – wakashangilia
Aliposema wanafuta sherehe za Ubunge kuokoa hela – wakashangilia
Aliposema wanafuta sherehe za Uhuru kuokoa hela – wakashangilia
Aliposema wanafuta kadi za Krismasi kuokoa hela – wakashangilia
Aliposema ataunda Baraza dogo la mawaziri kuokoa hela – wakashangilia
Alipopangua na kuwawajibisha wafujaji na kutaka hela irudi – wakashangilia
Alipokataa nyongeza ya posho zao za Ubunge kuokoa hela - wakashangilia

Kote huko walishangilia kwa sababu ilionekana hata kidogo kinachookolewa ni bora kuliko kufuja au kutumia pasipo ulazima. Walishangilia kwa sababu ilionekana kweli serikali inataka kutumia fedha kidogo za walipa kodi vizuri.

Hadi lilipokuja suala la wao kutoonekana kwenye TV! – Duh! Ugomvi!
Wanasema bilioni 4 mbona kidogo tu hizo kuzitumia kwa mwaka. Kwamba bilioni 4 kuangalia “live” kitu hicho ni gharama ambayo tuilipe tu ili tuwaone Bungeni!

Hawashangilii tena, wamekasirika, wamenuna! Wanataka waonekane “live”. Hata kwa bilioni 4! Kupunguza fedha kwenye mambo mengine yote ilikuwa ni kutekeleza ilani “yao”; lakini kupunguza kwenye hili ‘duh’ sasa ni “udikteta”.

Haikuwa udikteta kufuta sherehe za Uhuru? Haikuwa udikteta kufuta kadi za Krismasi? Haikuwa udikteta kufuta safari za nje? Haikuwa udikteta kuchukua fedha za tafrija ya wabunge kwenda kununua vitanda? Haikuwa udikteta kwenye kubana matumizi kwingine kote isipokuwa kwenye wabunge kuonekana “live” bungeni?
Kuna kitu hakiko sawa. Wachache tumekiona na tunakisema!


Hongera Raisi magufuli
 
Bilioni 4 hizo hizo zinazookolewa kwa kutoonyesha live kipindi cha bunge ni kiasi kinacholingana na kile ambacho tulikiokoa siku ya uhuru na kimewezesha barabara ya Bagamoyo kuanza kukarabatiwa. Nadhani ilichotakiwa kufanya serikali ni kuzipangia majukumu halafu yakajulikana kwa kila mtu, pengine uamuzi huo unaweza kuwafanya wakaelewa nini maana ya kubana matumizi. Kila mtanzania ni mwanasiasa, sawa sawa na ile hadithi ya kambale, baba ana ndevu, mama ana ndevu na watoto wote wana ndevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…