Joachim J Lyimo
Member
- Jun 16, 2013
- 74
- 16
Maisha ni ya thamani kubwa sana. Hata hivyo maisha huambatana na changamoto moja kubwa. Watu hupata maisha(kuzaliwa) wakati wakiwa hawayahitaji na wala hawajui thamani yake, na huyapoteza wakati yakiwa ndiyo kitu cha pekee wanachokihitaji. Kuna watu waliouza kila kitu, wakakimbilia hospitali bora Asia, Ulaya na Amerika wakiwa na matumaini ya kuongeza maisha(muda wa kuishi) ambapo wengine waliishi japo kwa kitambo, wengine walifikwa na mauti wakiwa hospitalini chini ya uangalizi wa matabibu na wengine walifia njiani kwamba ni mbali ama karibu tu katika safari yao ya kusaka matibabu.
Tafiti zinaonyesha kwamba vifo vigi katika siku za hivi karibuni vimekuwa matokeo ya mtindo usiofaa na chaguzi mbaya katika maisha. Kwahiyo wengi hupoteza maisha kwa kukosa ufahamu sahihi kama yasemavyo maandiko ya kwamba 'watu wangu wanaangamia kwa kukisa maarifa'.
Ukiachana na ajali ambazo mara kwa mara zimejimilikisha maisha ya wapendwa wetu, magonjwa ya mtindo wa maisha nayo hayapo nyuma katika kutwaa maisha yao. Wakati mwingine maisha hutwaliwa taratibu sana kiasi cha kutupumbaza hata tusing'amue sababu hasa za kukoma kwa maisha hayo.
Pamoja na kwamba watu wengi hupata japo mlo duni katika mazingira yao, lakini mara nyingi kile kinachopatikana hakitumiwi kwa usahihi. Watu hawaketi chakulani kuupatia mwili kile unachohitaji lakini mara nyingi lengo huwa ni kukidhi tamaa zao. Haishangazi kuona wimbi la watumiaji wa sembe na vyakula vingine vilivyokobolewa likiongezeka.
Watu wanaifanya chipsi kuwa mlo wao wa muhimu. Sukari ikikosekana karibu kila familia inalalama. Sembe, chipsi, sukari na vingi vya namna hiyo vina madhara mengi kwa watu wetu. Ni siasa isiyo na tija kuwashawishi watu kung'ang'ania visivyo vya muhimu. Usiponielewa naomba ufahamu kwamba babu zetu waliishi vizuri bila umeme ama TV. Leo kwa bahati mbaya vimefanywa vitu vya muhimu na vikikosekana watu wanaona karaha.
Watu wetu wangepaswa kupatiwa elimu ya kutumia vyema vyakula vinavyopatikana katika mazingira yao kwa ustawi wa afya zao na za kizazi kijacho. Wataalamu wa lishe wangepaswa kufanya warsha mbalimbali kusaidia watu wetu kutumia vyema chakula kinachopatikana kirahisi kwenye mazingira yao.
Kumekuwa na wimbi la kutisha la matumizi ya pombe na madawa ya kulevya kwenye jamii zetu. Kwamba ni ulanzi, mnazi, gongo, mbege, ama nyinginezo lakini madhara yake yamekuwa makuwa kwa utu na ustawi wa watu wetu. Kama taifa tumegoma kuitambua pombe kama madawa ya kulevya. Kahawa pia. Wakati pombe ikifanya kazi ya kuuzima mfumo wa fahamu, kahawa kwa upande mwingine huchochea. Kanuni inataka watu wasitumia madawa haya kwa wakati mmoja.
Bahati mbaya watu wetu hawana ufahamu juu ya hilo na wengi wamekuwa wakitumia vilevi hivyo kwa pamoja ama kwa kupokezana. Hadithi za nguvu za kiume huko Rombo na madhara ya kutisha ya kiafya katika jamii ya wachaga ingelipaswa kuamsha moyo wa kufanya tafiti na kusaidia watu wetu. Ifahamike kwamba afya ni kuwa timumu kimwili, kiroho, kiakili na kijamii.
Siku hizi kafeini inapatikana kwa wingi kwenye eneji drinki ambazo zinapatikana kila kijiji. Watumiaji wa pombe wako huru pia kununua bidhaa hizi zenye kafeini.
Kwa vyovyote vile, yapasa wataalamu wa afya ya jamii waamke, na kwa pamoja tuisaidie jamii yetu.
Watu wapewe elimu sahii ya ulaji na unywaji. Waelezwe kinagaubaga madhara ya moshi, sigara, bangi na madawa ya kulevya. Walindwe dhidi ya aina yoyote ya ujinga.
Taifa hili linamhitaji kila mmoja wetu. Afya yetu, nguvu yetu.