Mageuzi ya Kisiasa 2030

common buzzard

New Member
May 28, 2024
1
0
Siasa ya Tanzania imekua katika mdidimio mkubwa kuanzia 2020 na sababu kubwa ni kutokuwa na Demokrasia ya kweli, wakati wananchi wakitaka mabadiliko na mfumo mzima wa uendeshahi nchi wanasiasa wa upinzani wamegeuka na kuwa wasaliti kwa wananchi na kurudi upande wa chama tawala.

Wananchi wanatamani mabadiliko lakini wanasiasa wanayakataa mabadiliko.

Naiona Tanzania mpya kupitia kizazi cha 2000’s kutokana na upevukaji wao kifikra na kimaono na hii inachagizwa zaidi na ukuaji mkubwa wa sayansi na teknolojia.

Kufikia 2025 kwa kizazi hiki cha 2000 ni wazi kitakuwa tayari ni cha vijana wanaotaka maendeleo yao binafsi na ni wengi kwa takwimu hivyo kufikia 2029-30 ni watu wazima wenye kuweza kufanya maamuzi yao.

Hivyo kama serikali iliyopo itakuwa haijabadilika kwa mtazamo wangu naamini kizazi hiki kitawabadilisha.
 
Back
Top Bottom