vivaforever
Senior Member
- May 30, 2016
- 113
- 165
01. Gitarama Prison, Rwanda
Hili ndio gereza lenye msongamano mkubwa wa wafungwa Ulimwenguni huku likichukua wafungwa wapatao zaidi ya 7,000 huku lenyewe likiwa lina uwezo wa kuchukua wafungwa 400 tuu.
Wafungwa wengi ndani ya gereza hili ni washukiwa wa Mauaji ya Kimbari (Rwandan Genocide) ambayo yalitokea mwaka 1994. Sasa kutokana na msongamano mkubwa sana wa wafungwa, hawa Wanaume na Wanawake hulazimika kutumia mda mwingi wakiwa wamesimama peku (bila viatu) katika ardhi ambayo ni chafu kwa masaa yote ya siku, hii husababisha miguu yao kuoza.
Wengi wao hulazimika kukatwa miguu, lakini mbaya zaidi ni kuwa Gereza zima lina Daktari mmoja tuu wa muda wote. Wafungwa wengi wanashindwa kupata matibabu yaliyo sahihi hapo ndipo idadi kubwa ya vifo inaripotiwa kila uchwao.
02. Camp 22, North Korea
Hoeryong Concentration Camp, pia inajulikana kama "Camp 22," ni kituo ambacho bado kinafanya kazi tangu 1965, lakini kilifanywa kuwa siri kwa miongo kadhaa hadi pale kilipokuja kupigwa picha na satellite na picha kuzagaa mitandaoni.
Camp 22 ni moja kati ya vituo vya kukusanyia watu vinavyokadiriwa kufikia 30 huko Korea Kaskazini. Inaaminika kuwa kituo hiki kina watu (wafungwa) zaidi ya 50,000 ikiwemo Wanaume, Wanawake na Watoto, kwa sababu kwa sera za Nchi ya Korea Kaskazini.. wanaweza kufunga familia au ukoo mzima kwa kosa la mtu mmoja tuu. Wafungwa wengi hawana Afya ya mwili, wanateswa pia wanatumikishwa kwenye mashamba na migodi kwa masaa 12 kwa siku ndani ya wiki nzima (12/7).
03. United States Penitentiary, Administrative Maximum Facility (ADX), USA.
Hili gereza pia linajulikana kama ADX Florence, Florence ADMAX, Supermax, au the Alcatraz of the Rockies, hili ndio moja ya gereza lenye ulinzi mkali ndani ya Marekani. Lilijengwa mwaka 1994, hili gereza linachukua wafungwa ambao wanaaminika kuwa nu hatari sana kwa usalama wa Dunia ikiwepo Bwana Ted Kaczynski ( Aliripua eneo la Umoja wa Mataifa ), Ramzi Yousef ( Anahusika kwa uripuzi wa majengo ya Biashara Marekani mwaka 1993 World Trade Center bombing ), na Zacarias Moussaoui (anahusika na shambulio la 9/11).
Wafungwa kwenye gereza hili hutumia masaa 23 ya siku nzima kila mmoja akiwa amefungwa kwenye chumba cha pekee (solitary confinement), ndani ya hivyo vyumba kuna samani za kutengenezwa kwa zege ambazo hazihamishiki (mf: Stuli, kitanda kilicho na godoro jembamba na meza).
Kimo cha madirisha ya vyumba hivi ni futi tatu tuu na upana na inch 4, na chakula huwa wanapewa kupitia vitundu vidogo kwenye madirisha ya chakula. Wafungwa hutoka kwenye vyumba vyao kwa saa moja tuu kwa ajiri la kujifurahisha pia husindikizwa na walizi wengi.
Hili gereza unaweza kusema kuwa ndio aina "Safi kabisa ya Jehanamu".
04. Rikers Island Prison, USA
Limeundwa na jela 10 tofauti ambazo zina Wanaume, Wanawake na Vijana, gereza la Rikers Island lina sifa ya kuwa na vurugu sana, rushwa na kuwafanyia unyama wa hali ya juu wafungwa wake, hasa wale ambao wana magonjwa ya akili.
Mwaka 2008, baada ya kupigwa hadi kuuwawa kwa kijana wa miaka 18 (Christoper Robinson), ikaja kugundulika kuwa wahusika wa tukio hilo ni wafungwa wenza ambao walikuwa ni sehemu ya "Mpango”, hii ni jamii ya siri iliyokuwa inaendeshwa na walinzi wa Gereza lengo likiwa ni kuwatumikisha wafungwa flani kama chombo cha kuwafanyia vurugu wafungwa wengine kama njia ya kuwafanya wafuate sheria.
Rikers pia ina kiwango kikubwa cha vyumba vya upweke (Solitary Confinement Rooms), huku vikitumiwa sana na idara ya kurekebisha tabia ambapo kwa hivi karibuni vimejengwa vipatavyo 1,000 kwa ajili ya vijana na wale wenye magonjwa ya Akili.
05. Mendoza Prison, Argentina
Huku likiwa na idadi kubwa ya wafungwa (mara tatu ya uwezo wake), gereza la Mendoza ni nyumba ya vichaa. Wafungwa wengi mara nyingi zaidi ya watano utakuta wanaishi ndani ya kichumba kimoja tuu ambacho ukubwa wake ni mita za mraba 4 tuu.
Na kutokana na kutokuwepo kwa mfumo sahihi wa utoaji taka gerezani, wafungwa hulazimika kutumia mifuko ya plastiki na chupa kama vyoo vyao.
Mbaya zaidi ni kuwa hakuna mfumo wa huduma za Afya ndani ya gereza hili.. mda pekee ambao mfungwa anapokwenda kuonana na Daktari ni pale anapokufa tuu.
06. Diyarbakir Prison, Turkey
Diyarbakir Prison ni gereza lililo na kiwango kikubwa cha ukiukwaji wa haki za binadamu. Hii nyumba ya mateso inatoa mateso ya kimwili na kiakili (Physical & Psychological Tortures) kila siku, hii huchochea wafungwa wengi kujiua.
Pale familia zinapotembelea gereza hili huwa hazitakiwi kutamka neno lolote kwa sababu chochote kitakachotamkwa kitatumiwa kama njia ya kumtesea mpendwa wao.
Ingawa hili gereza limejengwa ili kuchukua wafungwa wapatao 700 tuu (Wanaume na Wanawake maeneo tofauti), mara nyingi huwa lina idadi kubwa ya wafungwa kuliko uwezo wake.
07. La Sabaneta Prison, Venezuela
Hili gereza ambalo lina idadi kubwa ya wafungwa lina zaidi ya wafungwa 3,700 ambao wanaishi kwenye eneo lililobuniwa kuchukua wafungwa 700 tuu.
Msongamano mkubwa kiasi hicho huchochea kuzuka kwa vurugu na magonjwa ya mripuko miongoni mwa wafungwa.
La Sabaneta linasifika kwa kuongozwa na mfumo wa rushwa ambapo walinzi hutoa upendeleo kwa wale ambao wana nguvu na pesa. Hawa wachache wenye nguvu huwa na uwezo wa kulala kwenye vyumba vyenye vitanda, wakati wengineo wotr hutumia machela kama vitanda kwenye korido.
Pia gereza hili halina miongozo ya kila siku, wafungwa hufanya kama watakavyo jambo linalopelekea vurugu za kila siku.
08. Terre Haute, USA
Hili gereza linapatikana huko Indiana linajumuisha vitengo vya ulinzi mkali 24/7, ulinzi wa kati na ulinzi mdogo. Hili gereza limepewa jina la utani "Guantanamo ya Kaskazini”, Terre Haute ndio gereza ambalo chumba cha kuulia wafungwa waliohukumiwa kifo na mahakama kinapatikana.
Wafungwa ambao wanatarajia kuuliwa (Death row inmates) huwa wanaishi ndani ya vyumba maalumu ambapo huwa wanafungiwa ndani ya vyumba vidogo kila mtu pekee yake na hufunguliwa mara tatu tuu kwa wiki ili watumie vifaa vya kufanyia mazoezi.
Hili gereza ndio bwana Dzhokhar Tsarnaev, muhusika wa uripuzi wa mabomu katika tukio la mbio za Boston (The Boston Marathon) anaishi kusubiri hatma yake ya kifo.
09. San Quentin State Prison, USA
Ndio gereza la zamani zaidi huko California, San Quentin linafahamika sana kutokana na vurugu zake.
Hili gereza limekuwa makazi ya wahalifu maarufu wengi ikiwemo Charles Manson, Scott Peterson na Sirhan Sirhan, ambao walihusika katika mauaji ya Robert F. Kennedy.
Katika jimbo la California, hili ndio gereza pekee lenye vyumba za kuulia wafungwa (Execution Chambers) kwa wafungwa wa kiume ambapo hutumia gesi yenye sumu kwa ajili ya kuulia.
10. Guantanamo Bay, Cuba
Linapatikana huko Mashariki ya Cuba, hili gereza linamilikiwa na Marekani na lilifunguliwa 2002 likiwa na lengo kuu la kuwafunga magaidi (Al-Qaeda & Taliban) hasa wahusika wa shambulio la 9/11 ambao watakamatwa huko Afghanistan.
Ingawa raisi Obama kipindi cha Uchaguzi aliahidi kulifunga hili gereza, lakini bado linafanya kazi kama kawaida hadi leo huku likiwa na wafungwa wapatao zaidi ya 150 waliogawanywa kwenye vikundi viwili (Camp Delta na Camp Iguana).
Pia kulikuwa na kitengo kingine cha muda mfupi kijulikanacho kama Camp X-Ray, lakini kilifungwa mwaka 2002, wafungwa kwenye kitengo hiki walikuwa wanapewa mateso ya hali ya juu kama vile kuzamishwa majini na kuvurugwa mfumo mzima wa fahamu.
K A R I B U N I
Sent using Jamii Forums mobile app