Magereza ya Tanzania kuwa katika hali mbaya, ni kwa sababu ya umasikini au kukosa utu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
6,822
9,657
Kwa nchi zilizoendelea, mtu kukaa gerezani humaanisha kukosa uhuru tu, lakini mahitaji mengine karibia yote ya muhimu huyapata.

Watanzania waliowahi kufungwa gerezani nchini walishasimulia mikasa na mateso waliyokutana nayo gerezani. Ni hali mbaya sana. Wafungwa hawajaliwi kama ipasavyo mwanadamu kujaliwa.

Na hilo ni tatizo la miaka mingi.

Hali hiyo inasababishwa na umasikini au kutokujali kwa watawala?
 
1722014282776.png
 
Kwa nchi zilizoendelea, mtu kukaa gerezani humaanisha kukosa uhuru tu, lakini mahitaji mengine karibia yote ya muhimu huyapata.

Watanzania waliowahi kufungwa gerezani nchini walishasimulia mikasa na mateso waliyokutana nayo gerezani. Ni hali mbaya sana. Wafungwa hawajaliwi kama ipasavyo mwanadamu kujaliwa.

Na hilo ni tatizo la miaka mingi.

Hali hiyo inasababishwa na umasikini au kutokujali kwa watawala?
Masuala yote yanayohusisha utendaji kazi wa askari Tanzania tumerithi mfumo wa kikoloni., sio gerezani tu hata katika ukamataji wa watuhumiwa hali ni iyo iyo, unaweza ukajisalimisha au ukatoa ushirikiano na bado ukapewa kipigo.
Nafikiri kuna shida katika aina ya mafunzo ambayo askari wanapewa uko makambini.
 
Ingependeza kama Zanzibar, tuiite "VYUO VYA MAFUNZO'

Nilipata kuhudhuria kozi ya mafunzo ya kurekebisha wahalifu nje ya nchi na nikapata maarifa. Hawa ni wenzetu ila tunawatenga kwa muda, wanapaswa kufanya kazi na kuzalisha. Kule Norway mfungwa analipwa mshahara. Hapa TZ wafungwa wanafanya kazi nyingi za nguvu, lakini ni kama wanawafanyia watu, wao hawalipwi. Tukiwatumia vizuri wafungwa uzalishaji utaongezeka, magereza yetu yana maeneo makubwa ya ardhim lakini hayatoi matokeo bora. Hakika Magerezani kuna Ma-Profesa, Ma-Doktori, Ma-MasterMind, Ma-KILAKITU...Hawa lini tunawatumia? NIPENI MWIZI NIMTENGENEZE KUWA MWIZI WA FAIDA KWA NCHI,AKIBE TEKNOLOJIA NJE YA NCHI...Haya weeee!
 
Aisee,hata mtaani waweza kataa kurudi
Nilishawahi kusimuliwa kuwa kulikuwa na Watanzania waliotaka kukatalia mahabusu ya Botswana baada ya kukamatwa kwa kosa la kuingia nchini humo kinyume cha taratibu. Walipokuta kuku ni sehemu ya mlo wa mahabusu, walitamani waendelee tu kukaa humo mahabusu.
 
Majority ya wananchi kitaa hata kupata basic needs tu ni shida (watu wanakupa milo miwili kwa siku tatu (alafu unaongelea wafungwa hawajaliwi )? Kumbuka hawa ninawaongelea walipa Kodi ambao wanakuwa shortchanged na watunga sera...

Kabla hatujaongelea kunywa wine atleast tuwe hata na maji ya kunywa...
 
Back
Top Bottom