Magereza ni kwamba mmekosea au ndo tarehe zenu zipo hivi?

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
3,122
4,995
Nimepata kukutana na picha inayoonesha kalenda Jeshi la Magereza, kalenda ya mwezi wa Oktoba na kukutana na tarehe 32 Oktoba 2024.

Screenshot_20241031_232852_X.jpg

Je, ni kwamba wamekosea au wapo sahihi!?
 
Nimepata kukutana na picha inayoonesha kalenda Jeshi la Magereza, kalenda ya mwezi wa Oktoba na kukutana na tarehe 32 Oktoba 2024.
View attachment 3140097

Je ni kwamba wamekosea au wapo sahihi!?
Wamekosea, hawako makini.

Ili mradi na wewe uonekane umepost ...makosa madogo kama hayo unatujazia server.
Hapana, yupo sahihi kwa hili.

Hii inaonyesha wazi kwamba Watu ambao wamekabidhiwa mamlaka katika nchi hawako makini kabisa katika kufuatilia mambo au hawako serious ktk kuzingatia majukumu yao waliyokabidhiwa.
 
Ili mradi na wewe uonekane umepost ...makosa madogo kama hayo unatujazia server.
Inategemea perspective ya mtu/jamii, lakini sidhani kama hilo ni kosa dogo. Kuna kipindi lilitolewa jarida la UDSM likiwa na neno Proffessor, yaani yenye double f, chuo kikalizuia kusambazwa. Kwa mwingine hilo lingeonekana kosa dogo, ila kwa chuo wao waliona wamefanya kosa kubwa
 
Na lilikuwa kosa kubwa
 
Haina shida yoyote mboona kuna dini muda huu wao ni mwaka elfu moja mia nne na kitu?!!
 
Labda waliona ni gharama kubwa kuchapa kalenda yenye usahihi wakaona bora hiyohiyo yenye makosa iendelee kutumika. Hela wanayo wakachape nyingine hiyo yenye makosa waitupilie mbali
 
Magereza kifungo cha miaka 30 unatumikia miaka 20 yaani 1/3* Miaka unaiondoa.

Usikute kwao siku 32 za kalenda kwao ni 31.
 
Back
Top Bottom