Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,822
- 5,429
Ukiachilia mbali Zanzibar kushusha viwanja vyenye hadhi ha kidunia. Sasa serikali ya Zanzibar ina mpango wa kushusha Treni za Kisasa, TAXI za baharini, na Mabasi ya Umeme (Electric Rapid Transit Buses). Ukubwa wa nchi ya Zanzibar unaingia zaidi ya mara 10 kwenye ukubwa wa mkoa wa Morogoro, Zanzibar ni ndogo sana, nchi ikipangiliwa vizuri itakuwa bora zaidi kimaendeleo kwa sababu kiutekelezaji eneo la nchi ni rahisi kulimudu. Zanzibar kiukweli chini ya Rais mwinyi inaonesha kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Wazungu ukiwauliza unafahamu nchi ya Tanzania, wengi hawajui, ila ukiwauliza wanaifahamu Zanzibar wengi watakwambia ndio.
Wakati huo huo, Tanzania bara haina hata Project kubwa ya maana Tangu yule mzee wa Chato aende zake. Kiukweli yule Mwendazake alipiga Project kubwa kubwa tu ndani ya Miaka 5 tu, Bwawa la nyerere, Meli kubwa na ya Kisasa pale ziwa Victoria "MV Mwanza Hapa Kazi Tu", daraja la Magufuli Mwanza, Barabara, Serikali kuamia Dodoma na Kuijenga Dodoma kuwa ya Kisasa. Na mambo kadha wa kadha bila kusahau kupambana na watu wenye vyeti feki, Kuanzisha sera ya Elimu bure, kupambana na madawa ya kulevya na rushwa, na kufufua Tanzania ya Viwanda. Jambo lilipolekea kupewa Jina la Bulldozer. Na mwamba kapiga haya matukio ndani ya kipindi cha miaka 5 tu, vipi kama angedumu miaka 10. Wengi walisema Investors wanakimbia nchi eti kwa sababu sera za Magufuli sio rafiki kwao, lakini cha kushangaza tuliona maendeleo, ila hivi sasa tunaambiwa Investors wameongezeka na mambo kadha wa kadha, lakini kodi ndio zinazidi kuongezeka. Sasa kazi ya hao investors ni nini hapa nchini wakatu maendeleo hayaonekani na tozo zinazidi songa.
Hivi sasa nikikuuliza nitajie Project mpya ya maana iliyopo Tanzania bara, uwezi kutaja hata moja. Sana sana utataja alizoacha mwenda zake. Apumzike kwa Amani, chuma alikuwa chuma kweli, anakwambia mimi kwangu tajiri anafanywa chochote. Huu msemo wa ukiwa na cherehani mbili wewe tayari una kiwanda ulisaidia kuwapa moyo wapambanaji wadogo wadogo, machinga na mama ntilie. Akasema pia Baa zote zifungwe mpaka jioni 😂, walevi tukanuna ila hatukuwa na jinsi.
Sasa hivi nikitazama Tanzania, sioni project za maana, tofauti na Tozo tu.
Haya ni maoni yangu, natimiza wajibu wangu wa kikatiba wa Freedom of Expression bila kuvunja sheria za nchi.
View: https://www.instagram.com/p/C1ySctJIl9j/?igsh=cnd4YjNrMXdpejM1