Magari ya petroli kutouzwa Ulaya ifikiapo mwaka 2035

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,178
Umoja wa Ulaya leo umependekeza marufuku ya uuzaji wa magari yanayotumia petroli na dizeli itakapofikia mwaka 2035. Pendekezo hili ni sehemu ya pendekezo kubwa la kimazingira litakaloharakisha kugeukia matumizi ya magari yanayotumia umeme ambayo hayatoi gesi ya aina yoyote.

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imependekeza kwamba ifikiapo mwaka 2030 gesi chafu ya kaboni inayotolewa na magari itapunguzwa kwa asilimia 55, lengo hilo likiwa juu zaidi ya lile lililopo sasa la kupunguza gesi hiyo kwa asilimia 37.5 ifikiapo mwaka huo. Halmashauri hiyo pia imesema ifikiapo mwaka 2035 magari yanayotumia petroli na dizeli hayatouzwa tena katika nchi za Umoja wa Ulaya hivyo gesi chafu ya kaboni kutoka kwenye magari itakuwa imeondolewa hewani kwa asilimia mia 100.
 
The future is exciting kweli. Kinachosikitisha ni kwamba Africa Africa tutaendelea kuwa wasindikizaji. In FACT, point ni kwamba hiyo 2035 magari ya diesel na petrol hayatatengenezwa tena. Hapo hujasikia plans za Japan na wengine wanakuja na mikakati gani. Sisi tutakuwa wageni wa nani? viongozi wetu waamke. COVID ime-expose umasikini wetu vibaya. Tumebaki kulalamika kwamba wakubwa wanahodhi chanjo! Bila kuwa na mchango wowote kwenye utafiti na utengenezaji wa hizi chanjo.

Tujipange..tukiendelea na hizi siasa cheap cheap...tutaendelea kuumia na kurithishana umasikini kizazi hadi kizazi.
 
... msajili a.k.a mlezi wa vyama vya siasa ameitaka Chadema ijieleze ni kwanini iliwafukuza wabunge 19 almaarufu Covid-19. Hayo ndio mambo tunayaweza Afrika!
 
Nao wanajua dunia inavyoenda, Saudi wana Vision2030, kupunguza utegemezi wa mafuta kwenye uchumi. Moja ya mission ni kuhakikisha watu wanaenda sana kuhiji-Utalii wa kidini.
Saudi wamechelewa kuamka na kupenda kujifanya wakali sana na mambo ya dini itawapa tabu kubadilika.... U.A.E wako mbali sana... kama Dubai ndio wamejijenga nje kabisa ya maswala ya mafuta sasa hivi.
 
UAE wana akili sana... walianza muda mrefu kuji-detach their economy from petroleum.

Umeme unazidi kuwa cheap hasa hasa Solar na Wind plus kuna Solid State Battery zinakuja. Toyota wako kazini wanakuja na gari ya 1000km range na Charge mpaka 80% kwa dk 10.

The furure is exciting
Gari gani hiyo?
 
Dunia inaenda kasi sana na kwa mtindo huu sisi ndio hivyo tena tutaendelea kuwa masikini zaidi kwani hatuna chochote tunachoongeza katika dunia hii.

Watu waliokuwa wanafanya exploration ya gesi kule Mtwara, Magufuli kaja kawavuruga wakaenda zao Mozambique, mwisho wa siku tutakuja kuambiwa eti gesi nayo sio mali tena.

Baadaye kwa kuwa na hizi serikali zetu hazina ubunifu watakuja kubandika kodi kwa mifugo, kuku na hata ile kodi ya kichwa itarejeshwa tena ili kuokoa serikali isifilisike.
 
Back
Top Bottom