- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nakumbuka shule niliyosoma tulikuwa tunawekewa mafuta ya taa kwenye chakula,
Katika kudadisi kwa nini watuwekee mafuta hayo niliambiwa kuwa wanatuwekea ili kutufanya tusiwe na hamu au kupunguza hamu ya kufanya mapenzi ukizingatia wanafunzi wanakuwa wameanza au walishapevuka tayari.
JamiiCheck naomba mnijibu, je ni kweli yanapunguza hamu ya kufanya mapenzi au walikuwa wanatulisha bure tu?
Katika kudadisi kwa nini watuwekee mafuta hayo niliambiwa kuwa wanatuwekea ili kutufanya tusiwe na hamu au kupunguza hamu ya kufanya mapenzi ukizingatia wanafunzi wanakuwa wameanza au walishapevuka tayari.
JamiiCheck naomba mnijibu, je ni kweli yanapunguza hamu ya kufanya mapenzi au walikuwa wanatulisha bure tu?
- Tunachokijua
- Mafuta ya taa ni kimiminika kinachozalisha nishati baada ya kuunguzwa ambayo hutumika sehemu mbalimbali. Kisayansi, mafuta ya taa ni nishati inayotokana na mafuta ghafi ya petroli.
Katika mchakato wa kubalehe baadhi ya homoni maalum hutolewa ambazo kimsingi ndizo huibua mabadiliko ya kimaumbile (secondary sexual characteristics) ili kuwawezesha vijana kuwa na uwezo wa kusababisha/kushika mimba (kuzaliana). Moja ya homoni hizo ni testosteron ambayo husababisha kuongezeka kwa ari ya kufanya ngono, upanuzi wa viungo vya uzazi kama vile uume na korodani, uzalishaji wa mbegu za kiume, ongezeko la misuli n.k. (kwa wavulana).
Kumekuwa na madai kuwa baadhi ya shule za sekondari za bweni huwa wanaweka kiasi kidogo cha mafuta ya taa kwenye chakula cha wanafunzi ili kuwapunguzia mihemko au hamu ya kufanya mpenzi.
Je, ni kweli Mafuta ya taa hupunguza Mihemko?
JamiiCheck imepitia Tafiti mbalimbali ili kubaini ukweli juu ya mafuta ya taa kupunguza Hamu ya kufanya mapenzi ambapo tumebaini kati ya tafiti zote zinaonesha kuwa hakuna ushahidi wa kisayansi juu ya madai ya Mafuta ya Taa kupunguza hamu ya kufanya Mapenzi.
Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa Kenya kufuatilia kiwango cha testosteron kwenye damu, utafiti ambao ulitumia panya dume wanaolingana uzito walio na umri wa wiki 6 ambao ndio kipindi chao cha kupevuka (balehe). Panya hao waliopewa mafuta ya taa walionesha kuongezeka kiwango cha homoni ya testosteron kwenye damu huku ambao hawakupewa wakibaki na kiwango kilekile cha awali.
Kwa mujibu wa Tovuti ya National Library Of Medicine ya Nchini Marekani imechapisha majibu ya utafiti ambao unaeleza kuwa Matumizi ya mafuta ya taa kwenye chakula katika shule za bweni yamekuwa ni jambo la kawaida nchi nyingi kwa miaka mingi, kwa imani kuwa hupunguza hamu ya kufanya mapenzi (libido) katika hatua ya kubalehe. Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuthibisha imani hii.
Aidha, tovuti ya mwananchi ilichapisha mahojiano waliofanya na madaktari wa binadamu ambao walieleza kuwa chakula kinapowekwa mafuta ya taa husababisha ongezeke la kutolewa kwa homoni ya testosterone ambayo huibua mabadiliko ya kimaumbile (secondary sexual characteristics) ambayo husababisha kuongezeka kwa nia na ari ya kufanya ngono, upanuzi wa viungo vya uzazi kama vile uume na korodani, uzalishaji wa mbegu za kiume na hata ongezeko la misuli.
Kwa mujibu tafiti hizo zinaeleza kuwa mafuta ya taa yalionesha kusababisha ongezeko la chembechembe nyekundu za damu (red blood cells) japo wameeleza kuwa mafuta ya taa huweza kusababisha kuvimba tumbo, pamoja na madhara mengine kiafya na kushauri kutumia njia mbadala kama kufanya mazoezi badala ya mafuta ya taa.