Mafunzo ya JKT yanaleta uzalendo?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
7,190
10,313
Inawezekana sijui kwa usahihi tafsiri sahihi ya neno uzalendo. Lakini najua dhima mojawapo ya kuwepo kwa mafunzo ya JKT ni kujenga uzalendo kwa vijana wa Tanzania!

Hilo lengo limefikiwa?

Mimi naamini Mzalendo hachukui rushwa. Naamini Mzalendo hawezi kuihujumu nchi yake!

Lakini mbona kuna watu walishawahi kuwa "masoja" kabisa lakini ni wala rushwa wa kutupwa? Mafunzo hayakuwakolea?

Najua mafunzo ya JKT yana faida, yanawaandaa vijana kwa nyakati za dharura! Ni kama Jeshi la akiba.

Lakini kwa tafsiri halisi ya uzalendo, JKT imefanikiwa?
 
Uzalendo ni wa watu ambao wapo tayari kufa kwa ajili ya nchi yao
Kufundishwa unyenyekevu, kuwa na upendo na nchi yako
Kuwa na mapenzi ya kujitolea kwa kila kitu kwa ajili ya nchi
Unakataa mabaya yote kwa kusimamia nidhamu
Yote haya kama wanafundishwa kwa nia njema basi tutarajie vijana wanaolipenda taifa lao na hawatapokea hata rushwa
Au wanajimba visiki tu na kuimbishwa nyimbo zisizo na faida kwao?
 
Inawezekana sijui kwa usahihi tafsiri sahihi ya neno uzalendo. Lakini najua dhima mojawapo ya kuwepo kwa mafunzo ya JKT ni kujenga uzalendo kwa vijana wa Tanzania!

Hilo lengo limefikiwa?

Mimi naamini Mzalendo hachukui rushwa. Naamini Mzalendo hawezi kuihujumu nchi yake!

Lakini mbona kuna watu walishawahi kuwa "masoja" kabisa lakini ni wala rushwa wa kutupwa? Mafunzo hayakuwakolea?

Najua mafunzo ya JKT yana faida, yanawaandaa vijana kwa nyakati za dharura! Ni kama Jeshi la akiba.

Lakini kwa tafsiri halisi ya uzalendo, JKT imefanikiwa?
Kama kujiunga na mafunzo ya jkt yanaleta uzalendo. Viongozi wengi wanafuja mali ya umma ndio hao waliopitia jkt
 
Back
Top Bottom