Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,662
- 8,787
Mafundi waliopelekwa nyumbani kufanya ukarabati au ujenzi wa nyumba wametumia mwanya huo kuchora ramani na kukariri vitu mbalimbali kwenye nyumba hiyo, pale waliposafiri na kumuacha housegirl wakavamia na kumuua kisha kufanya wizi.
Hiko ndicho kilichotokea Morogoro Mjini kwenye nyumba moja iliyokua kwenye ujenzi ambako Mafundi ujenzi watatu waliokua wakiijenga, wamekamatwa kwa tuhuma za kumuua Mfanyakazi wa kazi za ndani (House girl) Monica Paul (22) na kisha wakaiba vitu mbalimbali vya ndani.
Polisi Mkoani Morogoro wamethibitisha kuwashikilia Mafundi hao watatu ambao wote ni Wakazi wa Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za mauaji hayo ya Monica waliyoyafanya kwa kumnyonga April 14 2024 katika Mtaa wa Lukuyu Kata ya Bingwa Morogoro Mjini baada ya Mwenye nyumba kusafiri.
Kamanda wa Polisi Morogoro Alex Mkama amesema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi walifanya upelelezi na kufanikiwa kuwakamata WatuhumIwa hao watatu na wamekutwaa wakiwa na vitu mbalimbali vilivyoibwa katika nyumba hiyo ikiwemo TV na subwoofer pamoja na simu.
Kamanda Mkama amewataja Watuhumiwa hao kuwa ni Mbaraka Omary (25) Mkazi wa Tubuyu, Mussa Mrisho (23) Mkazi wa Bingwa na Rehema Omary (30) Mkazi wa Mwembesongo ambaye amekutwa na simu ya marehemu.