Mafundi simu wa upande wa hardware naomba tukutane hapa

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,916
kazi ya hardware ni ngumu sana na yenye lawama nyingi.

kuna simu unaweza ukaifungua ukaifunga na ikagoma kuwaka na wakati huo mteja alileta umbadlishie mic tu. na ukatemgeneza ugomvi mkubwa na mteja na akasema umembadilishia saketi na mnaweza kufikshana hata polisi mteja kama sio muelewa.

tatizo linakuwa wapi?

inamaana wakati unaifungua hiyo simu ulitoa betri bila kuzima simu. kwahiyo unapo toa betri hakikisha unazima simu.
na ikizima hivyo solution yake simu inatakiwa iende ikaflashiwe.
lakini tatizo lingine hawa mafundi software wanatuangusha sana mafundi hardware huwa hawataki kukomaa kabisa na wanapenda kazi rahisi rahisi na sijajua tatizo nini kwamba mazingira yanawabana au vipi.
kwasababu wao simu nyingi ukiwapelekea za kuflash. wanakuambia memory imekufa au kwenye computer haisomi lakini ukipima njia za usb ziko safi.

kazi ya hardware inahitaji akili yako zaidi tofauti na majamaa wanao deal na software wao kila kitu wanagoogle.

sisi upande hardware kuna baadi simu hata ugoogle vipi huwezi kupata solution hasa hizi tecno.

na ktk matatizo ya simu ambayo yanawatesa mafundi simu ni haya matatizo ya tecno.
na hii tuseme ukweli tecno na simu ya kimaskini na ndio maana kila mtanzania mwenye kipato cha chini anakimbilia.
na tecno ni simu ambayo matatizo yake ni pasua kichwa na ndio maana tatizo lolote ukiwapelekea tecno wenyewe wanakimbilia kubalisha saketi.

mm ni fundi ambaye natengeneza simu nyingi ambazo mafundi huwa wanzangu wanazishindwa.

siri ya ufundi simu.

1 ni kujua kuitumia mita vizuri 2 kujua kutumia gani vizuri 3 kuwa msafi 4 na kuwa mkweli.


kuna baadhi simu za tecno ambazo mafundi simu walisha kata tamaa kwamba hazi tengezeki lakini leo nitawapa baadhi ya solution kadri muda utakavyo kuwa unaniruhusu.
na kama hata ww utakuwa unasolution yoyote tutaomba tuzidi kusaidina.

tecno h5 p5 m3 hizi simu zimekuwa na tazizo sugu ukitaka kuiwasha tu inakuwa inajiminya button ya kujifomart

lakini mm kadri ya uwezo wangu nilijitahidi kugungundua solution ya hii tecno m3 kwa 100%.

na leo nataka nianzie hapo baadaye nitaleta solution
za tecno

fake charging tecno h6 l5 l6 tecno c8 c5

harafu nitaleta solutiona ya mic ya tecno ya tecno t340 na tecno zote zina zinazotumia system ya chaji ya v3

na hizo solution huwezi kuzipata pale na zamani tulizoe solution kutoka india lakini hizo simu india hazipo kwahiyo waafrika tukomae.

 
Ila Mungu anasaidia tunazipata maswala ya usb isipo detect mafundi hardware si mpo so ishu ni ushirikiano


Hah hah hah mkuu jana tu nimetoka kuflash simu ya Tecno nyingine m3 ilikuwa ukiiwasha inaishia katika LOGO.

Sijui ndio matatizo yake maana nyingi nimekumbana nazo.

Sasa wakati wa kuflash jamaa wa Software akasema Usb haisomi,nikamjibu mbona iko fresh kwa kuwa sikuifunga na screw nikaifungua nikacheki na mita iko powah jamaa akaichukua akagusisha gani katika njia ya njia upande wa GND akachomeka ikagoma nikajifanya niko bize akamnong'oneza jamaa yake kuwa haina tatizo sema niyakushikilia alafu baadaye akanambia hoyaa inabidii uongeze pesa si unajua nimechomelea nikabaki namuangalia tu.


Akaflash nikampa chake nilivyofika kibandan kwangu nikachek alipo choma nikabaki nachekaa hongera kwenu mafund Softwaree ila sisi ni wao mkuu
 
Tatizo hili ishu yake huwa tuna iflash kwa kutumia scatter file ambayo unatakiwa uwe na firmware ya hiyo sim,
 
Kama ambavyo ili uwe fundi mzuri wa hardware mbali na uzoefu inapendeza usome koz fupi ya eletronik


Vipi katika Software inapendeza usome kozi ipi.

Mkuu
Mm nilisoma computer engineering, so nilisoma vingi kuhusu technology, swala la software za sim ckuwah soma darasani vitu vingi nimejifunza baada ya kuface matatizo mpk kujikuta fundi mzur, i am good at computer software na hardware kuliko sim
 
Mm nilisoma computer engineering, so nilisoma vingi kuhusu technology, swala la software za sim ckuwah soma darasani vitu vingi nimejifunza baada ya kuface matatizo mpk kujikuta fundi mzur, i am good at computer software na hardware kuliko sim
Mkuu usichoke na maswali,


Una mda gani katika kuface matatizo ya simu?


Na je kuna kozi inayojihusisha na software za simu?

Kwa Dar
 
Mda mrefu nimeanza face hizi shida toka nikiwa second year chuo 2012, nikipata tatizo nilikua nikipitia forum tofauti tofauti ili kupata soln, kiukwel hakuna coz yyt ya ufundi wa simu, ila tu ni kua na idea za electronics kwa upande wa hardware na kujua lugha na majina na namna yakutumia software za sim
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…