Mafufu: sheria ya ndoa ibadilishwe katika vipengele vya ugawanaji wa mali baada ya talaka

9867_

JF-Expert Member
Jan 28, 2024
669
1,306
Hoja ya kubadilisha sheria ya ndoa, hasa kwenye vipengele vya ugawanyaji wa mali baada ya talaka, ni mjadala unaoweza kuibua hisia tofauti na mitazamo mingi. Katika jamii yetu, ndoa ni taasisi muhimu inayoheshimiwa na sheria zetu. Hata hivyo, pale ndoa inapovunjika, suala la ugawanyaji wa mali linakuwa ni la kihisia na la kisheria.

Hivi karibuni, kauli ya kiongozi na msemaji wa wasanii Bw. Jimmy Mafufu iliyosambaa sana katika mitandao ya kijamii imeibua mjadala kuhusu haja ya kurekebisha sheria ya ndoa, hasa kwenye vipengele vya ugawanyaji wa mali baada ya talaka. Yeye alipendekeza kwamba baada ya talaka, mali zote zibaki kwa ajili ya watoto. Sasa Je, hii ni suluhisho la haki na lenye manufaa kwa wote wanaohusika (mume, mke na watoto)?



Hapa ikatokea mitazamo miwili tofauti, wapo waliounga mkono juu ya sheria hii kubadilika na wapo walioona sheria iliyopo inajitosheleza. Nitataja baadhi ya hoja za pande zote mbili.
Hoja za kukubali Kubadilisha Sheria:​
  1. Maslahi ya Watoto: Waunga mkono wanadai kwamba watoto wanapaswa kuwa kipaumbele katika ugawanyaji wa mali. Kwa kuweka mali kwa ajili yao, kutahakikisha kwamba wanapata msingi thabiti wa mali na kiuchumi baada ya wazazi kutengana.​
  2. Mvurugano wa Familia: Pia, wanadai kwamba talaka inaweza kuleta mvurugano mkubwa kwa watoto. Kwa kuweka mali kwa ajili yao, kunaweza kupunguza athari za kisaikolojia na kijamii zinazoweza kutokea.​
  3. Usawa wa Ugawanyaji: Hoja nyingine kubwa ni kwamba, sheria ya sasa haitoi usawa wa kutosha katika ugawanyaji wa mali, hasa ikizingatiwa mchango usio wa kifedha kama malezi ya watoto na kazi za nyumbani, zinampa mwanamke sifa za kugawana mali ya mumewe hata kama haja changia chochote katika upatikanaji wa mali hiyo.​
Hoja za kupinga Kubadilishwa Sheria:​
  • Mchango wa Wanandoa: Wapingaji wa mabadiliko haya wanadai kwamba, sheria ya sasa inazingatia mchango wa kila mmoja katika upatikanaji wa mali. Hii inahakikisha kwamba haki za kila mmoja zinalindwa, ikiwa ni pamoja na mchango usio wa kifedha (kama inavyopingwa vikali na wanaotaka mabadiliko, nanilivyoeleza katika hoja yao ya 3).​
  • Desturi za Jamii: Pia wanasema, sheria inatoa nafasi kwa mahakama kuzingatia desturi za jamii, ambazo zinaweza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu umiliki wa mali baada ya ndoa. Hivyo, ipo fair.​
  • Madai ya Mali: Wanadai pia ya kwamba, kubadilisha sheria kunaweza kusababisha migogoro ya kisheria kuhusu nani ana haki ya kudai mali hizo kwa niaba ya watoto, hasa kama watoto bado ni wadogo.​
Je, tunawezaje kuhakikisha kwamba sheria inatoa suluhisho la haki na lenye manufaa/Maslahi kwa wototo na wanandoa wenyewe? Je, kuna njia mbadala ambazo zinaweza kuzingatiwa ili kuhakikisha maslahi ya watoto na haki za wanandoa zinalindwa?​
 
Usawa wa Ugawanyaji: Hoja nyingine kubwa ni kwamba, sheria ya sasa haitoi usawa wa kutosha katika ugawanyaji wa mali, hasa ikizingatiwa mchango usio wa kifedha kama malezi ya watoto na kazi za nyumbani, zinampa mwanamke sifa za kugawana mali ya mumewe hata kama haja changia chochote katika upatikanaji wa mali hiyo.
Daah hii kweli tena kama yamekukuta ndo utaelewa zaidi. Kimsingi Jamaa ana hoja ni basi tu kashindwa kuipangilia, mfano hilo la kusema mali zibaki kwa watoto HAPANA kwakweli
 
Daah hii kweli tena kama yamekukuta ndo utaelewa zaidi. Kimsingi Jamaa ana hoja ni basi tu kashindwa kuipangilia, mfano hilo la kusema mali zibaki kwa watoto HAPANA kwakweli
Yamekukuta nini mkuu😀
 
Sheria haina usawa ikitokea mwanamke ndiyo mwenye mali mwanaume anapunjwa sana au anaweza asipate hata huo mgao kabisa.
Hii sheria inaonekana ilitungwa kwa shinikizo la mwanamke wakati wa kujamiiana na mwanaume mwenye mamlaka fulani na mwenye ushawishi katika kutunga sheria na alipewa sharti akishindwa kuleta sheria hiyo kula tunda ndiyo basi tena.
 
Sheria haina usawa ikitokea mwanamke ndiyo mwenye mali mwanaume anapunjwa sana au anaweza asipate hata huo mgao kabisa.
Hii sheria inaonekana ilitungwa kwa shinikizo la mwanamke wakati wa kujamiiana na mwanaume mwenye mamlaka fulani na mwenye ushawishi katika kutunga sheria na alipewa sharti akishindwa kuleta sheria hiyo kula tunda ndiyo basi tena.
Sheria si inatungwa na bunge mkuu🌝?
Screenshot_20240530-164924.jpg
 
Bunge linapitisha tu hatuna bunge linalotunga sheria nchi hii.
Waziri au mwanasheria mkuu wa serikali anapeleka muswada bunge linapitisha kama ulivyo yamekwisha.
Mawaziri wao kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanatengeneza muswada. Muswada sio sheria, ili uweze kuwa sheria ni lazima bunge lliridhie na Raisi apitishe.
IMG_20240530_170740.jpg
 
Mawaziri wao kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanatengeneza muswada. Muswada sio sheria, ili uweze kuwa sheria ni lazima bunge lliridhie na Raisi apitishe.
View attachment 3003848
Na mimi ndicho nilichosema kwamba bunge linapitisha tu sasa kama umeliona hilo sijui tunabishana nini!
Na Rais yeye anaridhia baada ya bunge kupitisha sio kinyume chake.
 
Back
Top Bottom