SoC04 Maendeleo katika Sekta ya Michezo Tanzania ndani ya miaka 15-20 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

docha de brigher

New Member
Jun 1, 2020
2
0
Awali ya yote nipende kutoa pongezi kwa timu mbalimbali za michezo pamoja na wawekezaji wake hapa Tanzania( Simba na Yanga) zimejitaidi kadri ziwezavyo kulitangaza soccer la Tanzania kwa kila namna ziwezavyo na zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa saana, japokua timu hizo zinafanikiwa kutokana na uwekezaji zinaoufanya lakini sifa pamoja na matunda mengi ynarejea katika aridhi ya Tanzania 🇹🇿 sababu ndipo zinapotokea timu hizo.

Tanzania tuitakayo katika sekta ya michezo miaka 15_20 Ijayo !
1. Maendeleo ya timu ya taifa katika kufuzu mashindano mbali mbali na kuwa sehemu ya kujivunia kama watanzani.

2. Uboreshaji wa viwanja mbalimbali vya michezo ilikuweza kuondoa utata kwa marefaree pindi wanapokua katika viwanja hivyo kuamua hizo mechi.

MAPENDEKEZO NA MKAKATI YA KUFIKIA HAYO MAENDELEO YA SEKTA YA MICHEZO NDANI YA MIAKA 15_20 IJAYO.

Shirikisho la mpira nchini yaani TFF wakishirikiana na Serikali kwa ujumla waweze kuunda na kuanzisha academy za michezo za Taifa zisizopungua kumi (10) kama mwanzo wa kuibua chachu ya soccer katika timu ya Taifa la Tanzania 🇹🇿.

Taifa la Tanzania limebarikiwa vijana wengi saana wenye vipaji vya soccer. Ukiangalia kuanzia shule za msingi na mpaka Sekondari , vijana wenye vipaji vya mpira ni wengi saana , tatzo ni namna ambavyo serikali na shirikisho la mpira Tanzania wanakosa mikakati ya kuwatumia vijana hao ili kuleta maendeleo ya michezo katika timu ya Taifa.

Uanzishaji wa academy za timu ya taifa za mpira katika aridhi ya Tanzania,
Inatakiwa uchukue vijana ambao bado wabichi ( hawajafikia umri mkubwa) na kuweza kuajili wakufunzi walio bobea katika michezo ( football coach) pamoja na wasidizi wako.

Academy hizo za timu ya taifa , zitafundisha ndani ya miaka 10 hadi 15 huku zikiendelea kupokea challenge tofauti kutoka katika timu tofauti tofauti na kuendelea kupima uwezo wao siku hadi siku ili kuimarisha ubora wa wachezaji hao.

Huo utakua mwendelezo wa soccer la Tanzania , yaani vizazi na vizazi , miaka na miaka hizo academy za Taifa zitazidi kuchanua na kutoa vinaja walio bora na watakao liwakikisha taifa la Tanzania katika sekta ya michezo na kuendelea kupeperusha bendela ya Nchi mahala popote kimichezo 🇹🇿.

Hakika baada ya mikakati hiyo na mapendekezo hayo kufanyika , 90% ya soccer la Tanzania hususani timu ya Taifa litachanua na kuoneka katika sura tofauti kabisa na mataifa mengine kimichezo.

Na hii itapelekea viwanja vya michezo kuweza kubadilika kuoingana na quality ya wachezaji, wawekezaji, quality ya soccer la nchi na board ya michezo pamoja na serikali kiujumla na kuitangaza Tanzania kimataifa katika sekta na michezo na kupelekea kukuza maendeleo mengine ya Nchi.
 
Back
Top Bottom