Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Jeshi la Nigeria linasema karibu wanamgambo 6000 wa Boko Haram wakiwemo makamanda , wapiganaji na familia zao wamejisalimisha kwa mamlaka katika muda wa wiki chache zilizopita.
Cameroon pia ilikuwa imetangaza kujisalimisha kwa mamia ya ya wanamgambo Boko Haram nchini humo hivi karibuni.Jeshi la Nigeria linasema kujisalimishwa kwa wingi kwa wanachama wa Boko Haram kunatokana oparesheni kali ya kijeshi inayoendesha dhidi ya wanamgambo hao kaskazini mashariki mwa nchi.
Kifo cha kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau mwezi Mei huenda kumechangia hali hiyo.
Baadhi ya wafuasi hao huenda wamejisalimisha kwa mamlaka au walijiunga kundi pinzani la wapiganaji- Islamic State Afrika Magharibi, ISWAP.
Mamlaka nchini Nigeria zinasema sasa wanatoa wasifu kwa wale ambao wamejisalimisha kwa lengo la kuwapa ushauri nasaha.
Lakini Wanigeria wengine wana wasiwasi juu ya kuwaunganisha tena wapiganaji wa zamani katika jamii- wakitaja hatari zinazoweza kutokea.
Kulingana na Umoja wa Mataifa uvamizi wa Boko Haram ulianza 2009 -umesababisha vifo vya watu 300,000 na mamilioni ya wengine kuachwa bila makao Nigeria na nchi nyingine kadhaa katika eneo la Ziwa Chad.