Madudu ya APP za mikopo online.Wizara husika Mnakazi gani ofisini??? #Wizara ya Fedha #Wizara ya Mawasiliano (TCRA)

De Professor

JF-Expert Member
May 21, 2021
236
495
Kwa Niaba ya Wadau wananchi wa kawaida kabisa nadhani ni wakati sahihi wa kupazia sauti kadha hii ambayo imefumbiwa macho kwa muda mrefu na vyombo vyetu husika.

Week chache zilizopita niliamua kuvalia njunga swala moja la mtu ambae alikua akidaiwa na App moja ya Mtandaoni ikiitwa *SUNN LOAN ndipo nikapata kufahamu madudu mengi ya App nyingine nyingi za aina hii zinazojinasibu kutoa pesa online kwa mashart kidogo na kwa haraka zaidi.
Ilianza namna hii:-

Week tatu zilizopita nilipokea simu kwa namba ya Airtel +255 696 448 617 kijana akajitambulisha kuwa wakala wa kampuni ya mikopo Sunny Loan na akasema mimi ni mmoja wapo wa watu walio orodheshwa na mteja wao kama rafiki wa mteja wao alieshindwa kulipa deni lao la Tsh 71,000/= kwanza nilishangaa maana mtu aliemtaja kiukweli kwa wakat huo wala sikua namfahamu na nilimjibu kwa ukali kidogo nikimwambia simfahamu na wala sijawah shirikishwa kwenye mambo hayo, sauti ya huyo kijana alisema sawa ila naomba umwambie alipe Pesa yetu au Umlipie .
Kwa kipindi hicho nilipuuzia maana nilihisi huenda wamekosea namba au ni matapeli.
Baada ya siku hiyo nilianza kupokea jumbe zao za msg wakimdai huyu mtu na kunitaka niwasiliane nae nilipoona wapo serious nilimtafuta huyo ndugu na alimielezea kilichomsibu.

Concern yangu inaanzia hapa:-
Baada ya kuona hivyo nilimpigia simu na nikamhoji kwa kina imekuaje anadhalilishwa namna hiyo na kama kweli alikopa kwanini asilipe maana Dawa ya deni nikulipa.
Naunga mkono kwa kusema kulipwa ni haki yao ikiwa walimkopesha ila baada ya kufanya research nimegundua ujanja ujanja mwingi unaopelekea either mtu ashindwe kurejesha kwa wakati au pengine pesa aliyokopa na aliyooneshwa kurudisha imeongezeka zaidi.

Mdaiwa alinijuza kuwa deni alilokopa ni Tsh 33,000 tu na ilitakiwa kurejesha 51,000 Tsh ndani ya siku 7.
Ajabu baada ya siku 5 tu alitumiwa simu ya kutaka kurejesha mkopo wake iliyofuatiwa na simu iliyopigwa na mtu akijitambulisha kua wakala wa Sunny loan akiulizia marejesho ndipo akamjibu siku ya marejesho bado.
Baada ya siku 7 hiyo siku alikwama kulipa na kesho kutwa yake Deni likawa 53,000 yaani amepigwa faini ya 2000 Tsh. na kwa kua alikua akiwa na nia ya kulipa baada ya kutafutwa aliomba kulipa kwa awamu yaani instalment ambapo kila baada ya siku 7 alitakiwa kulipa 17,850, lakin katika awamu hizi atatakiwa kulipa awamu 4 yani kwa kulipa 17,850 ×4= 71,400.
Hapo ndipo waliposhindwana na kurushiana maneno yasiyofaa kwanini alipie 71,400 badala ya elfu 51, au elfu 53,000/= ambazo wanasema amepigwa faini?

Huyu ndugu akasema yule wakala hakutaka mjadala badala yake alisema kama hutalipa ndungu zako watazilipa.
hapo ndipo alipoanza kutafutwa na watu mbali mbali nikiwepo mimi, na kuna wengine wanamyumia msg zilizotumwa na hao watu wa kampuni, hivyo akasema Deni alikwisha lipa la elfu 53,000/= ila hao watu wamekua wakishinikiza alipe zaid.
Mara ya kwanza nilihisi ananidanganya lakin nikaja kuthibitisha aliponionesha Account yake ya sunny loan iliyoonesha alikopa 33,000 na akalipia 53,000/=
Rejea picha no 1. ipo hapo inaonekana.
20240725_160017.jpg



Basi kuanzia hapo nikaanza kuzifatilia hizi App za online maana hata sikuwah zifahamu, siku moja nili google nikaona watu wamezizungumzia Pesax, Maisha Bora, Twiga loan etc na wakawa wanalalamika sana namna walivyotendwa.
Hakika ukiwa na marafiki wengi sio ajabu kujikuta unahusishwa na mikasa hii hata zaidi ya mara 1 au 3 ndani ya miez michache.

Leo nimecheka sana baada ya kujikuta nimewekwa kwenye group la whatsapp la mtu anaetuhumiwa kudaiwa 42,000/= ghafla nimejikuta mimi na watu wengine 7, huku picha ya group ni huyo mdaiwa na maelezo ya kuhusu kudaiwa kwake.
Rejea picha no 2, ya jina Vera.
huyu pia nimejaribu kumuuliza yeye kasema jina la App ni #Mkopo Fasta

20240725_153559.jpg


Nilipomuuliza kwanini hajalipa nayeye stor yake haipishani kwasababu katika hiyo 42,000 anayodaiwa alikopa 30,000 tu na akapewa 25,000 iliyoingia kwenye simu yake maana nyingine ilikatwa juu kwa juu hivyo kimsingi ni alikopa 25,000 badala ya 30. na kutakiwa kulipa Tsh 40,000/= alipoingia kwenye account akakuta anatakiwa kulipa 42,000/= alipoanza kuhoji na kusema atafanya malipo baada ya kueleweshwa ndipo akawekwa kwenye group la whatsapp na watu wake.

MASWALI YANGU KWA WIZARA HUSIKA:-
1. Inakuaje haya makampuni yanakopesha kwa Riba kubwa namna hii? na kutoa pesa ki ujanja ujanja mfano yule anaoneshwa amekopeshwa elfu 30, ila inaingia kwenye simu elfu 25. na riba za kurejesha zipo vile vile na juu.

BOT na Wizara ya fedha haya hamja yafahamu au tuhisi wamepenyeza mbachao ?

2. TCRA mpo wapi mbona wananchi wana haribiwa haki yao ya msingi ya privacy? na wanakua black mailed kwa kosa la kuruhusu taarifa zao zidukuliwe na contacts zao zote kutambulika, je wamiliki wa App wapo sahihi kuingilia privacy ya mawasiliano ya mteja?
vipi utaratibu wao wa kudai siku chache kabla ya tarehe sahihi ya marejesho?.

Mimi sio nabii lakin kwa nilichokiona wakati nafanya reseach na kupitia review za app play store asilimia 85% walizungumzia vibaya App hizi na kuonya watu wasitumie haya napata kutabir kuwa kuna kundi kubwa la watu waliopata kadha hii.
Dawa ni kuto kukopa? Kulipa hivyo hivyo au Mamlaka husika isimamie uendeshaji sahihi na watu wanufaike na mikopo hii ya haraka ?
 

Attachments

  • 20240725_160017.jpg
    20240725_160017.jpg
    106.6 KB · Views: 14
  • 20240725_153559.jpg
    20240725_153559.jpg
    416.2 KB · Views: 15
  • 20240725_153559.jpg
    20240725_153559.jpg
    416.2 KB · Views: 15
Back
Top Bottom