Kutokana na TCU kutoa idadi ya wanafunzi wasio na sifa zaidi ya 8000 waliodahiliwa na tume ya wanafunzi wa elimu ya juu na kujiunga na vyuo mbali mbali hapa nchini hii imetosha sasa!
Ndalichako achia ngazi kwani haya madudu unayoyafanya kupitia TCU ni dhahiri kwamba wewe ni kikwazo kikubwa katika kuwaanda wanafunzi wenye ubora kulingana na mahitaji ya jamii hasa watakaoifanikisha Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati, hatuwezi fanikisha haya yote kama tunapeleka wanafunzi chuo kikuu wasio na sifa tena wanapewa na mikopo(pesa ya walipa kodi) huku wenye sifa na vipanga wakikosa mikopo hiyo.
Imetosha sasa, jiuzulu tu kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa. Hii pia itakujengea sifa wewe mwenyewe kwani kwa sasa huna uwezo wa kuikwamua elimu yetu hapa ilipofikia zaidi ya matamko!
Pumzika mama, bora ujikite katika majukumu yako kule familia tu.
Umewakumbatia wasio na sifa 8000 sasa imetosha, pisha wengine waendeleze wizara nyeti hii