Madikteta Wanazaliwaje na Wanakufaje?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,432
73,078
Sijasema nani ni dikteta ila napenda tujiulize hao madikteta wanazaliwaje (sio biological) na wanakufaje (wanavyoishia).

Mwaka 1971 Idd Amin alipo mpindua Obote utawala wake uliookelewa kwa shangwe na matumaini makubwa. Alipoamua kuwanyanganya waasia mali zao na kuwafukuza wananchi wakawa na matumaini makubwa kwake hivyo kila alilosema likaonekana kina nia njema kwa nchi yake.

Lakini Amin alikosa vision ya mwekekeo wa kiuchumi wa kuinua nchi na nchi ikaanza kuporomoka. Wanasiasa walipoanza kulisemea hilo akaona litampunguzia unaarufu, akawakamata na kuwafunga mwisho akaona isiwe tabu akaanza kuwaua. Hapo ndio Udijteta wake ukipozaliwa. Viongozi wa dini walipoona hayo wakakemea nao wakapandishwa vyeo kuwa marehemu.

Nchi ikagwaya, wataalamu na wanaharakati wakosoaji eitha wakanyamaza, wakakimbia nchi na waliojifanya mdomo unawasha yakawakuta makubwa. Maisha yakawa magumu, uchumi uka angamia kabisa na nachafuko juu. Ikawa hakuna njia nyingine zaidi ya kumtoa Amin kwa nguvu na hicho ndio kikawa kifo chake katika utawala.

Alijifia kwa aibu akiwa mafichoni Saudia. Ingekuwa ni zama hizi basi angeenda kuibuliwa huko Saudia na angefia jela.

Nani anachangia kuzaliwa na kufa kwa madikteta? Obviously ni wananchi wenyewe kugawanyika katika kusifu na kukosoa mienendo ya utawala wa binadamu huyo.
Sauti za kusifia zikiwa na nguvu na kuonekana zile za kukosoa zinatenda dhambi kuna jenga tabia ya huyo binadamu kuchukia ukosoaji.

Sasa kimbembe kitakuja pale hata wale wasifiaji watakapo anza kupungua kutokana binadamu huyo kushindwa kutumia ushauri mbadala na hali ya uchumi kuwa mbaya.
Ili ku maintain stutas binadamu huyo huanza kutumia njia mbalimbali kuzuia idadi ya wakosoaji kuongezeka na ndio MWISHO MBAYA humtokea mfano wa huyo Amin aliye ingia kwa shangwe na madikteta wengine.

Wananchi wanawezaje kujizuia kuzalisha hao madikteta? Nazungunzia hasa hapa Afrika.
 
Tukubaliane tu kuwa Mwafrika hajawa tayari kwa safari ya maendeleo hasa ya kweli.....bado anataka mchezo mchezo na upuuzi mwingi katika kila nyanja. Mwafrika hajawa tayari kuitazama mbele katika picha kubwa......anapotokea mmoja au wachache wenye mtazamo wa maendeleo halisi huyo hupigwa vita na wote walio ndani na walio nje. Hata ndani ya familia kukatishwa tamaa huja kwanza kabla ya kutiwa moyo.....watanzania sasa wako bize kukatisha tamaa kila juhudi ya kuibadili nchi.
 
Mkuu Chakaza, katika enzi hizi za 2010 na kuendelea usitegemee kuona dikteta akianza kufanya unyama halafu akaachwa tu aendelee kufanya awezalo. Kumbuka madikteta wengi waliweza kuwa na nguvu sana enzi zile za maisha ya sanduku la posta (SLP). Unatuma barua kwenda kigoma leo na inafika baada ya wiki mbili.

Dunia tunayoishi ambayo imejaa maisha ya smartphone na facebook, haiwezi kuvumilia kuzaliwa kwa tabia ya udikteta. Dhana ya udikteta haina nguvu katika dunia iliyojaa taasisi zinazotetea haki za binadamu, dunia ambayo ni kijiji kwa maana ya wepesi wa watu kufahamu yanayowasibu binadamu wenzao wanaoishi katika nchi mbalimbali.
 
Tunamuona Magufuli DIKTETA kwa Sababu ya hangover ya utawala wa JK. Lkn laiti kama Magufuli ndo angepokea kijiti kutoka kwa Mkapa ambaye ni kariba na role model wa Magufuli wala tusingeongea haya. Ukweli ni kwamba upinzani ulideka mno kwa JK. Hebu tukubali kuishi kama watoto wa kambo kidogo tuone kama hafai basi tunamwondoa madarakani maana si lazima kumaliza miaka 5. Wananchi kupitia Bunge wanaweza kumwambia Magu basi baba, inatosha. Ishia hapo.
 
Kwanini uzuie? Udikteta is inevitable when ufisadi situation is alarming
Kwani kuzuia ufisadi,wizi na ubadhilifu ndio udikteta? Au unachanganya maana mkuu?
Hayo si ni mambo yanayoshughulikiwa kwa sheria sio hapa tuu bali duniani pote.
Jerry Rawlings wa Ghana alipambana na hayo mambo kwa mkono wa chuma lakini hakuwahi kuitwa dikteta kwa nini? Ni kwa vile akikuwa anatumia sheria na sio utashi na aliheshimu katiba ndio maana kastaafu kwa heshima
 
Hapana...bahatimbaya kwa watanzania..u dikteta ndo lugha pekee mnayoielewa
 
Bunge lipi ? Hili la yes yes mzee?
 
Wanaofanya ufisadi wote wako ndani ya CCM na Srikali. Wapinzani waanike ufisadi huo wa kutisha na Serikali haichukui hatua zozote zile kwa sababu Kikwete ni fisadi na Magufuli ni fisadi wanahofia maovu yao kuanikwa na waliomo CCM na Serikali. Halafu wa kuwalaumu ni mafisadi eti wanadeka!!! Inaonyesha jinsi kiwango cha akili yako kinavyofanya kazi.

 
Ingekuwa hivyo basi tusingesikia kelele chungu nzima toka kwa Watanzania wanaojitambua kuhusu huyu dikteta uchwara.

Hapana...bahatimbaya kwa watanzania..u dikteta ndo lugha pekee mnayoielewa
 
Mtu akiwa mkali mnasema dikteta, akiwa mpole mnasema boya, kanywea, moto wa mabua e.t.c
Wabongo kwa kutia chumvi hamjambo..
 
Bungee la ccm, limejaaa ndioooooo hata penye hapana. Sahau
 
Vipi democrasia? Mbona MTU akihoji tu polisi wapo mlangoni?
 
Vipi lugumi, ESCROW, au ndio mwisho wa ukali.
 
Vipi lugumi, ESCROW, au ndio mwisho wa ukali.
Nimeamini ni vigumu kuujadili ufalme wa Mungu bila kutaja na kutafakari ufalme wa ulimwenguni kwanza.
Nia ya Uzi huu ikikuwa wananchi wanawezaje kuzuia kuzaliwa kwa nadikteta Afrika, lakini wadau naona wamegoma kujadili Afrika bali wamepiga about turn na wanachezea uwanja wa nyumbani tuu na kufanya uzi uchukue picha kwamba jee huyu ndiye au siye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…