Madereva wa Bolt wote hapa Tanzania kuna haja ya kuunda umoja wetu ili nasi kwa pamoja tusikilizwe changamoto zetu maana changamoto tunazopitia ni nyingi ila tunashindwa kupewa kipaumbele kwasababu hakuna anaepaza sauti kuhusu hizo changamoto.
Changamoto hizo ni kama:
(1)Kiukweli Bolt inampa kipaumbele sana Abiria kuliko sisi wafanyakazi wake
(2)Tunafanya safari ndefu kwa hela ndogo sana
(3)Safari za usiku zinakuwa na hela ile ile kama ya mchana wakati usiku usalama mdogo + usiku ni muda wa mapumziko.
(4)Kumfata abiria kwa umbali mrefu ambao umbali huo huwa hauhesabiwi/haujumlishwi kwenye hela ile utakayoipata kwa abiria
(5)Makato makubwa wakati sisi ndio tunaofanya kazi kubwa, tunanunua mafuta, tunanunua Oil, unanunua bando(mawasiliano + Mb) Bado changamoto zote kubwa na ndogo tunazimaliza wenyewe.
Kuna haja ya kuunda umoja ili changamoto kama hizi nilizozitaja hapo juu zidhibitiwe kupitia ngumu ya wengi.
Asanteni