Madereva malori wa kitanzania waporwa mizigo na kunyanyaswa DRC

Mateso chakubanga

JF-Expert Member
May 10, 2021
611
828
Katika hali inayostajabisha walitokea wahuni wa DRC wakasimamisha malori haswa yanayoendeshwa na kutoka Tanzania na kuanza kupora vitu vyao kuwashusha kwenye malori na kuwazuia kuingia ndani ya DRC
 
Majeshi ya SADC[Tz na SA] yalijisalimisha Congo...Waasi waliwaamuru lini waondoke, silaha gani zitoke, zitoke kwa namna gani na zitoke kupitia border gani.

Aibu ya karne.....sishangai wa-Congo kudharau madereva wanaotoka Tanzania.

Kuna mtanzania alikwama South Sudan week kadhaa sijui kama kasaidika. Alimgonga mwanajeshi akafariki...alikamatwa na polisi familia ikaamuru alipe fidia ya milioni 33. Sijui kama kasaidika...

Ukiachana na hilo....Madereva wawili wa watanzania walishambuliwa na wahuni Zambia....hadi tunaongea ni marehemu sasa.
 
Serikali yao inatakiwa itoke hadharani na kukemea huo uhuni.

Tanzania Kwa muda mrefu imekuwa ni mdau Mkubwa wa DRC

Tukisema nasisi tuwabanie hapo Bandarini hakuna kitu watafanya

Watu wenyewe Kila kitu wanaagiza kupitia Tanzania
 
Acha uongo hivi unajua Kinshasa ipo karibu ya taifa Gani kubwa ulaya
 
Tunahitaji mtu kama Bashe aje atie neno hapo Mzalendo pekee aliebaki ccm.

Oya Bashe eeh!! tia neno hapo kuna matembele humo kwenye maroli yetu!!!
 
kuna clip inaonesha mangi mmoja akibishana nao asee me sitoi sasa hii ni fedheha asee wengine tumeacha familia nyumbani,😂😂.

wacongo wakamtight akala kabari clip ikaishia hapo
 
Acha uongo hivi unajua Kinshasa ipo karibu ya taifa Gani kubwa ulaya
Sipo kwaajili ya kuonesha uongo wangu ama uerevu wako, ila ninachoweza kukueleza ni kwamba Kwa namna jiografia yao ilivyo.

DRC wanategemea bandari yetu Kwa zaidi ya asilimia 85

Hiyo Nchi ya Ulaya wanaweza kuwa na mahusiano ya kawaida ya mtu na boss wake lakini hakuondoi ukweli kwamba DRC wanategemea mno bandari zetu za Tanzania
 
Kwahiyo wewe vitu unavitoa mbinguni sio ulaya na kingine congo Haina bahari mpaka wakutegemee wewe Kila kitu
 
Naomba ujipe muda ukajielimishe kuhusu Nchi ya Congo na mipaka yake.

Upande wa mashariki tumepakana nao kupitia Ziwa Tanganyika ambalo na magharibi wamepakana na Nchi nyingine ambazo hazina bahari pia

Kwa urahisi wanatakiwa watumie bahati yetu ya Hindi katika kusafirisha mizigo

Ndiyo maana ukifika hapo Tunduma border utakutana na msululu wa magari ya mizigo yanaelekea DRC,Zambia na Nchi za Kusini
 
We umesema Kila kitu wanaitegemea tanzania ndio maana nikakuambia acha uongo
 
Kwahiyo wewe vitu unavitoa mbinguni sio ulaya na kingine congo Haina bahari mpaka wakutegemee wewe Kila kitu
Congo mizigo wanayoingiza hutoka Asia,bei nafuu,bidhaa za ulaya hawazimudu,wakiachana na bandari ya dar maana yake washushe Mombasa, mzunguko mrefu,au meli toka asia zizunguke misri zikapakue mzigo bandari yao kinshasa,bado gharama juu
 
Hao wahuni wa mtaani hawayajui hayo....
 
Back
Top Bottom