Deni la mkandarasi kwa Serikali limesababisha ujenzi wa jengo la tatu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kusuasua huku baadhi ya vifaa vikiwa vimekwama bandarini.
Mkandarasi huyo ambaye ni Kampuni ya Bam International ya Uingereza, anadai Sh21.4 bilioni huku mkandarasi mshauri akidai Sh1.8 bilioni na Sh279.7 bilioni zinadaiwa kwa ajili ya kukamilisha mradi huo, ambazo bado hazijapatikana.
Mradi huo ambao ulianza kujengwa mwaka 2013, unatakiwa uwe umekamiliaka Desemba mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salum Msangi amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 66 mpaka sasa.
Kaimu Mkurugenzi huyo alimesema hayo jana kwenye ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa aliyetembelea mradi huo.
Profesa Mbarawa amesema mradi huo utagharimu Sh560 bilioni hadi kukamilika kwake.
Chanzo: Mwananchi