Madawa ya kilimo na madawa wanyama Kuna shida mahali

hauleibrahim

Senior Member
May 17, 2024
183
122
Hivi naomba kujua na kufahamu madawa ya kwenye mazao na kilimo na mifugo huwa majaribio yake wanayafanyiaga wapi?

Kuna maduka mengi yanauza madawa ya mifugo pamoja na madawa ila haya madawa mengi yamekuwa hayana matokeo Bora Kwa wakulima na wafugaji.

Nikiwa kama mkulima n mfugaji na nikiwa n wafugaji wengine wengi tunakutana na hizo changamoto za kidawa.

Swali langu kubwa hizi dawa kama TBS huwa wanapitisha hizi dawa huwa wanazingatia nn?

Kama wana zingatia hicho kitu na kupitisha hizi dawa mbona hizi dawa bado ni changamoto sana Kwa mkulima shambani na Kwa wafugaji mifugo.

Unaweza tumia dawa kumi au 3 Shamba moja na usipate matokeo ya kueleweka hiyo hiyo hata kwenye mifugo madawa ni mengi ila yenye matokeo ni machache sana.

Je serikali hizi dawa wanazo zipitisha na kuzipatia tbs na hazina matokeo huwa wanazifanyia majaribio wapi kwenye mines gani na wanazingatia hali ya hewa gani?

Kuna dawa mathalani za kilimo SI ajabu inayo fanya kazi vizuri njombe isifanye kazi vizuri dar je huwa tunazingatia nn kupitisha dawa maan wakulima na wafugaji wanateseka sana kujaribu madawa mengi bila sababu huku matokeo yakiwa hayaeleweki kabisa.

Ni wakati sahihi watu wa tbs watuambie dawa za mifugo naza kilimo majaribio yao huwa wanayafanyia wapi na kuyaruhusu huku mitaani au mikoa mingine ambako matokeo chanya hakuna kabisa Kwa mkulima.

Kilimo na ufugaji sio vitu vigumu Kwa mtz yoyote ila ugumu inaletwa na watu wa mamlaka ya dawa hasa kupitisha dawa zisizo na matokeo Kwa mkulima na mfugaji wa kitanzania
 
Umejuaje kama shida iko kwao badala ya kwako wewe mtumiaji? Unazijua factors zinazofanya dawa ilete matokeo mazuri kwa mifugo?
 
Kwa ufupi Usimamizi wa Dawa Upande wa Kilimo na Mifugo ni hafifu.Taasisi zinazohusika kuruhusu uingiaji,Usajiri,usambazaji,wauzaji na Maduka husika kuna shida.
 
Moja ya majanga makubwa ni hayo kwenye eneo la kilimo na ufugaji na ndio ilipaswa iangaliwe sana maaana ndio chakula kilipo Serikali imeachia kila kitu kinaenda hovyo hovyo....

Kila mtu anafungua duka la dawa za kilimo na mifugo hata.kama hana utaalamu

.mfano tunazuia GMO lakini ukienda madukani zimejaa mbegu za GMO...
Baadae sasa magonjwa mengi ni kwasababu ya haya madawa..Mboga za majani kwa mfano mtu anapiga hizo dawa feki anaingiza sokoni kesho sasa tutakosa kansa?? Figo kufa??? Moyo kutanuka?? Watu wanaumwa sanaaaa...
 
Shida nimezijua ndo mana nimeandika ningekuwa sijui shida hata hili andiko nisinge Kaa chini na kuliandika.naandika kitu kilochopo nacho kutana nacho kama mkulima pia mfugaji.
Pia Factor za dawa yoyote kuleta matokeo ni kufuata maelezo husika ya matumizi ya dawa kama mtengenezaji anavyotaka itumiwe na mpka naandika manayake nimefanya hayo sijapata matokeo zaidi namaliza fedha kununua madawa tofauti tu huku matokeo yakiwa ni kisoda au nothing

Back
Top Bottom