Madaraka Ya Kulevya

Polandspring

New Member
Mar 27, 2017
3
0
Madaraka ya kulevya


Napenda kuanza kwa kujilaumu kwa kutokuwa kijana mwenye kuchukua hatua bayana katika maswali mengi ya kisiasa katika nchi yangu. Lakini kila kitu kinatokea kwa wakati wake muafaka na baada ya kuondoka nchini kimasomo nimekuwa nikifatilia mwenendo wa siasa Tanzania kama njia moja wapo yakunifanya nijihisi sipo maili 8000 kutoka nyumbani. Lazima niwe muwazi kuwa sijawahi fungamana na chama chochote kile cha siasa na msimamo wango katika chaguzi mbalimbali nikuchagua sera na sio chama. Baada ya kuongozwa kwa miaka takribani 50 na chama kimoja bado niliamini katika chaguzi ya mwaka 2015 na nilishiriki kumchagua mgombea wa chama tawala, Mheshimiwa John Pombe Magufuli.


Napenda kuendelea kuamini kuwa huu sio muda wa kutupiana lawama au kunyoosheana vidole na kusema nani alikuwa chama gani na kwa misingi gani. Uchaguzi ulikuwa huru na wakidemokrasia na sasa ni muda wa kuungana kulijenga taifa kwa pamoja bila kujali dini, rangi, kabila wala itikadi ya chama. Kama kuna kitu ambacho kila mtanzania inabidi ajifunze kutoka katika vitendo vya hivi karibuni vya Rais John Pombe Magufuli, ni kutudhihirishia kwamba, hakuna ‘huduma maalumu’ utakayopewa kwa kuwa tu ni mfuasi wa chama chochote kile. (Nape Nnauye)


Kwa jinsi ambavyo sakata la hili la Mkuu wa mkoa wa dar es salaam, Paul Makonda lilivoanza kiutani na hatimaye kufichua mambo ambayo kwa hali ya kawaida si rahisi kuamini yangeweza kutokea katika nchi yangu pendwa. Inasikitisha kuona kwamba kuna baadhi ya viongozi, wanasiasa na hata watu maarufu nchini wakifumbia macho jambo hili. Wengine wakiendelea kupotosha jamii kwa kauli za kipuuzi zenye kuwaacha wananchi wengi katika sintofahamu. (William Malecela)


Takribani wiki mbili zilizopita Mheshimiwa Paul Makonda (RC) alianzisha kampeni ya kutokomeza biashara ya madawa ya kulevya nchini. Hakika Madawa ya kulevya yamekuwa tatizo kubwa na ambalo ufafanuzi wake bado unachelea kupatikana. Idadi kubwa ya wananchi ilimuunga mkono na kupongeza uthubutu wake kulivalia njuga jambo hili. Kwa miaka kadhaa iliyopita tumeona watu waliojitoa kimasomaso kupigana vita hii ya madwa ya kulevya wakikutana na vikwazo kedekede mathali, kuuliwa, kufilisiwa mali zao, kumwagia tindikali nk.

Binafsi minongono iliyoanza kumuhusu Mkuu wa mkoa wa dsm kufoji vyeti vyake vya elimu ya juu niliichukulia kama jitihada za wahusika wa madawa ya kulevya kudidimiza juhudi za RC. Baada ya minongono hii ukaanza kuibuka ushahidi wa wazi na unaojitosheleza kutibitisha kuwa RC analala kitanda kimoja na hawa Ma‘don’ wa Madawa ya kulevya.


Lakini vita hii ilionekana ikiwalenga watu wachache mashuhuri nchini ambao ilisemekana kuwa RC hakuwa na mahusiano mazuri nao. Huu ulikuwa ni uvumi wa mtandaoni ambao ungeweza kuepukika endapo taratibu zingefatwa katika ukamatwaji wa hawa watuhumiwa wa madawa ya kulevya. Unaweza kuhoji juu ya mamlaka ya Mkuu wa mkoa kuwaita watuhumiwa katika kituo cha polisi central kwa mahojiano. Waweza kuhoji pia mantiki iliyotumika kuwapa watuhumiwa hao siku tatu wajisalimishe wenye kituo cha Central. Miongoni mwa waliotajwa ni wakiwemo Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Mfanyabiashara na Mmiliki wa Yanga FC Yusuph Manji, Wema Sepetu na Francis Ciza (Dj Majjay wa EFM Radio) . Sababu za watu hawa wote kukamatwa zinatofautiana na zinaweza kufanya Makala hii iwe ndefu zaidi. Lakini jambo linalozidi kunishangaza ni uamuzi wa mkuu wa mkoa kujiweka juu ya Mamlaka iliyoteuliwa kupambana na Madawa ya kulevya hadi pale ambapo wananchi wakapiga kelele juu ya uvunjaji wa itikadi za kiserikali katika vita hii.


Labda nirudi nyuma kidogo, utendaji wa namna hii wa kukurupuka na kufanya maamuzi ya kimhemko hayajaanzia kwa RC peke yake. Tangu kuanza kwa muhula wa tano wa Raisi JPM kumekuwa na ongezeko la viongozi mbalimbali wa serikali hii ikiwemo mawaziri, wakuu wa wilaya na hususan Raisi mwenye kutoa matamko ambayo hayana mantiki na yanayoshinikizwa sana na hisia za kwa papo kwa papo.

Ni jambo ambalo sasa linajulikana wazi kuwa RC ambaye kisiasa anaweza kusemekani ni kijana mdogo lakini ambaye ameonekana akifanya kazi kubwa sana katika jamii toka alipokua mkuu wa wilaya ya Kinondoni na kupelekea Raisi kumuamini na kumpa Ukuu wa mkoa. Bahati mbaya nikipenda kumnukuu Waziri Mkuu Mstaafu Bw Frederick Sumaye akisema kuwa labda uwezo wake ulikua umefikia mwisho, alikumbwa na kasumba ya kutafuta kiki katika vyombo vya habari.

Nafasi ya ukuu wa mkoa haihitaji uwe ni mhitimu wa darasa la saba sembuse chuo kikuu. Ni mamlaka ya kuteuliwa na Raisi kutokana na vigezo atavyoona vinafaa. Lakini hatuwezi kufumbia macho shutuma za kufoji vyeti vya elimu zinazoelekezwa kwa RC ambalo kisheria ni kosa la jinai.Na tumeona wafanyakazi wengi wa serikali katika nyanja tofauti wakifukuzwa kazi kwa kosa hilo hilo. Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi aliyekuwa madarakani kuhusishwa na hujuma kama hizi.

Mwaka 2005 Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe alishutumiwa na Mgombea wa NCCR Mageuzi Lazaro Matete kuwa anawadanganya wananchi na hajasoma. Zitto aliweka hadharani vyeti vyake na kuukata mzizi wa fitina daima. Pia mnamo mwaka 2016 Raisi Magufuli alimteua Bwana Luhende Pius kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi. Punde tu zikazuka tuhuma kuwa aliishia kidato cha nne na alikuwa Meneja wa Hoteli ya City Style Sinza. Raisi magufuli aliclarify story hii na kumuamuru Luhende aonyesha vyeti vyake vyote vya elimu.

Ukimya huu wa Raisi magufuli katika sakata la Paul Makonda unatia wasiwasi sana kwakuwa unaleta picha ya undumilakuwili kwa kiongozi wa nchi. Unaashiria dhana ya uongozi bora ambayo Raisi Magufuli amekua akihubiri katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu wa uongozi wake, ina chembechembe ya upendeleo kwa watu ambao ni maswahiba wake.
 
Hawa jamaa wawili Magu na Bashite nahisi kabisa wana ajenda zao za siri na msiri wa jpm huenda ni Bashite, na hizi safari za nje za bashite huwa siziielewi kabisa.
Makonda hana vyeti halali hilo ni dhahiri,
Swali la kujiuliza ni je wale waliachishwa kazi kwa kosa la kufoji vyeti wana uchungu kiasi gani kuona alie waachisha wao kamuacha mwingine aendelee.?
 
Back
Top Bottom