Madaraja kupanda ni kila baada ya miaka mitatu kwa watumishi wanaendelea na ajira,
Kwa watumishi wa ajira mpya(first appointment) hupanda daraja baada ya miaka 4
Hivyo, mwaka wa fedha 2016 /2017 wanaostaili kupanda ni wale waliopanda mara ya mwisho mwaka 2013 kurudi nyuma na wale walioajiriwa mwaka 2013.
Kama wewe umeajiriwa mwaka 2013 basi unapaswa kuwekwa kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 ili ikifika mwaka 2017 upande daraja na mshahara wako ubadilishwe.
NB:upandaji madaraja unategemea na ufanisi wako ktk kazi, nidhamu bora, ujazaji wa fomu za OPRAS, na uwepo wa fedha kwenye bajeti ya mwaka husika,