Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,959
- 13,727
Baada ya member wa JamiiForums.com kuripoti kuwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rutabo hawapewi Chakula cha Kutosha kutokana na uhaba wa Chakula na kudai kuwa hatua hazichukuliwi, Serikali imechukua hatua.
Awali member alidai Shule hiyo inawapikia Wanafunzi Chakula kidogo hali inayowalazimu kugombania na kuomba hela nyumbani mara kwa mara kwa.
Andiko liko hapa - Wanafunzi wa Rutabo High School (Kagera) hawapewi chakula cha kutosha
Afisa Elimu Sekondari Kagera, Michael Lugola amesema alimuagiza Afisa Elimu Kata ambaye ameenda kwenye shule hiyo na kumpa ripoti hii:
Nimefika katika Shule ya Sekondari Rutabo, tumefanya kikao na Wanafunzi tukawapa nafasi ya kueleza changamoto zinazohusiana na chakula.
Walichokieleza kilikuwa cha kawaida, sio kikubwa kama kinavyoripotiwa kwenye Mtandao, tatizo kidogo lilielezwa siku za Wali na Nyama kuwa wakati mwingine hawashibi lakini walikiri kuwa ugali unatosha.
Tumeweka mkakati mpya ikiwa ni pamoja na usimamizi wa chakula kutoka kinapokuwa stoo mpaka jikoni.
Kuongeza Walimu wa kusimamia na kuonja ubora wa chakula, kuongea na Wapishi ili kuhakiki wanaandaa chakula kizuri na kuhakikisha hakuna hujuma ya chakula sehemu ya jiko.
Wanafunzi viongozi kutoa taarifa ya mapungufu ya chakula kwa Mwalimu au Mkuu wa Shule haraka sana yanapojitokeza ili yafanyiwe kazi.
Na Mimi nimeahidi kufika mara kwa mara shuleni saa za Wanafunzi kupata chakula ili kujionea hali halisi.