Machi 11, 2020 WHO ilitangaza COVID-19 kuwa janga la Kidunia, unakumbuka nini kipindi katika janga hilo?

Mwenyezi Mungu amfute madhambi yote Dr. John J. Magufuli akampumzishe peponi Amina..
 
Miaka minne iliyopita Shirika la Afya Duniani WHO lilitangaza kuwa COVID-19 ni janga la Kidunia -pendamic disease.

Je, wewe unakumbuka nini kilichokusibu?

Mimi nilipoteza kazi yangu siku hiyo!
Viongozi wa kiserikali na wasio wakiserikali, ndugu, Jamaa na marafiki zangu wengi mno walipoteza maisha ndani ya kipindi kifupi sana 🐒

May Their Souls Rest In Eternal Peace 🐒
 
Nazikumbuka barakoa za kushona hasa vitenge na jinsi watu walivyokua wanazidhihaki na kudharau
 
Leo Kuna Mitaa Nimepita Nimekuta Gari Zipo Kwenye Maegesho Ndani Kuna Barakoa Zile Ambazo Box 1 Zilikuwa Zinauzwa Laki. Oops Nikawaza Hivi Dude Lipo?
 
Viongozi wa kiserikali na wasio wakiserikali, ndugu, Jamaa na marafiki zangu wengi mno walipoteza maisha ndani ya kipindi kifupi sana 🐒

May Their Souls Rest In Eternal Peace 🐒
Uko sahihi,watu wengi ambao niliwafahamu walikuwa wanaondoka kila kukicha,bahati mbaya mtu wangu wa karibu naye alipata,ilikuwa ni kipindi kigumu sana,hofu ilitawala,matumaini ya kuiona kesho yalikuwa yametoweka,ni neema ya Mungu tu tulisalimika...
 
Nakumbuka kuna Rais alitangaza kuwa hakubali chanjo na hatoweka watu wake ndani, hakika yalikuwa maamuzi sahihi.
 
Kilikuwa ni kipindi kigumu sana maana Mazishi yalikuwa kila sehemu lakini unazuiwa kusema kuwa ni Ugonjwa wa Corona unasema Changamoto ya kupumua.
 
The world can b a weird place.
Mimi nakumbuka Covid ilinipa advantage maana before it nlikua nmepauka vbaya sina kitu and at the same time nmeingia chuo kuongeza elimu. So nkaomba kazi jis for fun. Nkaipata but mkoa tofaut na shule.
Nkaenda kwenye training ya hyo kazi ili at least nipate hela ya training alaf nkalipie kodi. 2nd day of training wakatangaza kufunga vyuo.
So nkaenda kazini, and ended up kufanya kazi and school hadi nkamaliza.
Pole sana.
 
Rais wa sasa angekuwa ndio Rais wa wakati wa kipindi kile, Tanzania nzima tungeshinikizwa kuchanja chanjo ya corona, tena hata kwa viboko angetaka tuchanje..lakini ashukuliwe Mungu wa mbinguni aliyekuwa Rais wakati huo alikuwa imara sana na mtu wa imani kubwa sana...akatuvusha salama. Wengine katatizo kadogoo tu wameanza kuomba watanzania wachanje na vitisho kibao.....kweli mwanaume ni mwanaume tu :D
 
Hii COVID-19 ilipelekea nimepata katoto kwa sababu ya kufungia vyuo kwa muda. Sasa hivikana miaka 3 niko nako hapa kananiita baba kila dakika.
 
Back
Top Bottom