Machache yaliyoonekana Simba SC ikitandikwa na CS Costantine

kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
2,030
3,975
1. Jean Charles Ahoua hana hadhi ya kuichezea Simba, dirisha dogo timu itafute playmaker mwingine

2. Upangaji wa kikosi umeendelea kuwa tatizo kwa kocha wa Simba, kuwaanzisha kwa pamoja mabeki wa kati watatu kuliwapunguzia umakini katika kutimiza majukumu yao.

3. Timu imecheza vizuri zaidi baada ya Debora Fernandez kuingia, kama kikosi kingeanza hivi huku kikishambulia na kulinda kwa tahadhali, mechi ingemalizika kwa sare au ushindi kwa Simba.

Soma Pia: Full Time: CS Constantine 2-1 Simba Sc | CAF confederation cup| December 8, 2024

4. Lionel Christian Atebba ni mshambuliaji mzuri ila muda sio mrefu ataonekana garasa kama mchezeshaji ataendelea kuwa Jean Charles Ahoua (mechi ya leo ni mwanzo wa hiki)

5.Kocha wa Simba apunguze uoga akiwa ugenini alichokifanya leo ndicho alikifanya kwenye mechi na Al ahly tripoli, walio karibu naye wamwambie Simba ni timu kubwa jina tu linatosha kuzipa hofu timu pinzani hata zikiwa kwao.

All in all Nafasi ya kufuzu bado ni kubwa.
 
Hili suala la haka katoto AHUA nishasema Sana sema huwa sieleweki .........
Mpaka kamfukuzishe kazi huyu kocha haka katoto ang'oke nako.....

Sio mukwala wala Ateba wanaonekana wachovu kutokana na namba 10 wao namna anacheza kwangu big NO.......

Mara 100 tuwe na mtu kama Yacouba yule wa Tabora ni Bonge la playmaker sio haka katoto....

Naunga mkono hoja...
 
Kwani Ahoua sio ndo Top scorer ajaye au😂
Ahoua kwa namba anayocheza hana msaada kwa timu. Ni mchezaji liable / weak sana number TEN inatakiwa uwe jitu la mavitu na utulivu wa kutosha.

Kocha ana changamoto ya kupanga kikosi na hiyo ni kwa sababu ya kuamini kulinda zaidi na kukosa umakini langoni mwa mpinzani.

Ahoua kwa sasa ni mzigo kwa Timu kitendo cha kocha kumweka nje AWESU ni kutukosea mashabiki huyu mchezaji wake hana sifa ya kucheza hata Tabora United. Mchezaji hana hatari langoni mwa mpinzani utulivu zero , Passing zero & dribbling zero so what kind of professional player is this ?

Kocha anatukosea sana Simba fans AWESU yupo Deborah ana utulivu mzuri anaanzia benchi kweli ? Ahoua must Go anawakaba wenzake.
 
Madhara ya kuchukua wachezaji wa bei rahisi ndiyo haya
 
Sema wewe kaka walau usikike .....anawapa mateso Sana namba 9 zetu ....wanaonekana wa kawaida sababu mzigo unakua mkubwa Sana wa kupambana na mabeki ......
Kana tabia ya kukimbia dimba la juu kwenda pembeni .......nadhani anafaa kucheza kama kiungo wa pembeni na sio namba 10 .......
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko (Lialia) SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyaunyau (mapaka) SC.
8. Mwakarobo SC.
9. Mikia SC.
10. Miso Misonda SC.
11. Manyang'au SC.
12. Mazumbukuku SC.
13. Mazombi SC.
14. Kinyume nyume SC.
15. Ngada SC.
16. Kolowizard SC.
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Panya roads SC.
20. Kikanuni SC.
21. Kufa Kiume SC.
22. Ubaya ubwege SC.
23. 5imba SC.
24. Visingizio (Visababu) SC.
25. Manguruwe SC.
JamiiForums-751034406.jpeg
 
Kuna wakati unajiuliza iwapo hawa wachezaji wetu mpira ndio kazi yao au kuna nyingine wanafanya halafu mpira ni kazi ya ridhaa tu kwao. Kwanini mchezaji hakui? Yaani makosa anayofanya yanakuwa hayo hayo. Ahou amekuwa mchezaji anayefanya makosa yaleyale mara zote. Kadhalika Mutale, na wengine na wengine.
Hivi ni kweli hawa ukocha ni taaluma kiasi kuna ma model wanatumia au ni kama uganga wa kienyeji tu? Haingii akilini uwe na kikosi zaidi ya miezi kadhaa halafu usijue perfect combination yao uwanjani.
 
Sema wewe kaka walau usikike .....anawapa mateso Sana namba 9 zetu ....wanaonekana wa kawaida sababu mzigo unakua mkubwa Sana wa kupambana na mabeki ......
Kana tabia ya kukimbia dimba la juu kwenda pembeni .......nadhani anafaa kucheza kama kiungo wa pembeni na sio namba 10 .......
Yes.halafu kanatabirika,huwa kanakimbia pembeni halafu kanapiga chenga ya kufinya mpira kulia kwa nyuma ambayo inasimamisha au kupoozesha mashambulizi,halafu kanakimbia kivivu na mpira then hakatoi pasi kwa wakati
 
1. Jean Charles Ahoua hana hadhi ya kuichezea Simba, dirisha dogo timu itafute playmaker mwingine

2. Upangaji wa kikosi umeendelea kuwa tatizo kwa kocha wa Simba, kuwaanzisha kwa pamoja mabeki wa kati watatu kuliwapunguzia umakini katika kutimiza majukumu yao.

3. Timu imecheza vizuri zaidi baada ya Debora Fernandez kuingia, kama kikosi kingeanza hivi huku kikishambulia na kulinda kwa tahadhali, mechi ingemalizika kwa sare au ushindi kwa Simba.

Soma Pia: Full Time: CS Constantine 2-1 Simba Sc | CAF confederation cup| December 8, 2024

4. Lionel Christian Atebba ni mshambuliaji mzuri ila muda sio mrefu ataonekana garasa kama mchezeshaji ataendelea kuwa Jean Charles Ahoua (mechi ya leo ni mwanzo wa hiki)

5.Kocha wa Simba apunguze uoga akiwa ugenini alichokifanya leo ndicho alikifanya kwenye mechi na Al ahly tripoli, walio karibu naye wamwambie Simba ni timu kubwa jina tu linatosha kuzipa hofu timu pinzani hata zikiwa kwao.

All in all Nafasi ya kufuzu bado ni kubwa.
Hivi nyie mnazijuantimu kubwa kweli🤣🤣🤣🤣
Timu iliniwe kubwa africa lazima uwe umeshinda champions league ata mara moja mzeya sio kufika robo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom