Machache usiyoyajua kuhusu filamu ya "Kuch Kuch Hota Hai"

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,449
25,362
Kuch Kuch Hota Hai ni filamu iliyotolewa mwaka 1998, iliyoongozwa na Karan Johar ,imeigizwa na mastaa kadhaa kama vile Shah Rukh Khan aliyeigiza kama Rahul Khana , Kajol (Anjali Sharma) na Rani Mukerji (Tina Malhotra)na Salman Khan (Aman Mehra).

Filamu hii inahusu hadithi ya mapenzi na urafiki.
Wakati filamu hii inatengenezwa, Karan Johar alikuwa na miaka 25 na alipata msaada mkubwa kutoka kwa baba yake, Yash Johar, ambaye alikuwa mtayarishaji maarufu wa filamu kupitia Dharma Productions ambayo ni kampuni ya baba yake ndio iliyofadhili filamu hii
  • Karan alipendekeza nafasi ya Tina (Rani Mukerji) aigize Karisma Kapoor au Twinkle Khana lakini baadaye nafasi hiyo ilikwenda kwa Rani Mukerji baada ya Karisma na Twinkle Khana kukataa
  • Salman Khan alikubali kuigiza filamu hii kama Aman Mehra, bila malipo makubwa, kutokana na urafiki uliokuwepo kati yake na Karan Johar na Shah Rukh Khan.
Machache usiyoyajua kuhusu filamu hii .
1. Jugal Hansraj aliipata tune ya "Tum Paas Aaye" wakati anaoga, baada ya hapo akampa director Karan Johar

2. Shah Rukh Khan na Kajol walikuwa ni machaguo ya kwanza ya Karan Johar kucheza Rahul na Anjali. Walumuahidi kushiriki kwneye filamu yake hii ya kwanza tangu Karan alipokuwa muongozaji msaidizi (Assistant director) kwenye DDLJ.

3. Wakati filamu inafanyika Rani alikuwa na miaka 19, na kutokana na sauti yake kuwa ya kukwaruza bwana K-Jo alipanga mtu mwingine Kuja kuingiza sauti kwenye mazungumzo ya Rani baada ya kumaliza kushoot.

4. Wakati wa kushoot tukio la kuendesha baiskeli kwenye wimbo wa "Yeh Ladki Hai Deewana", Kajol alishindwa kui-control baiskeli yake, akaanguka kifudifudi, na kupoteza fahamu. Aliumia goti lake pia. Kuanguka kulikuwa kubaya kiasi cha kumfanya Kajol kupoteza kumbukumbu kwa muda. Mtu pekee ambaye aliweza kumkumbuka alikuwa mpenzi wake wa wakati huo ambaye sasa ni mume wake, Ajay Devgn.

5. Ingawa mavazi yake yalipendwa sana baada ya filamu kutoka, Shah Rukh alikiri kuwa alikuwa akijisikia aibu kuvaa mavazi yake katika filamu hiyo kwa kuwa alihisi yalikuwa yamebana sana.

6. Uhusika wa Aman ulitakiwa kuchezwa na Saif Ali Khan, lakini aliikataa. Baadaye, Salman Khan alimfuata KJo kwenye sherehe iliyoandaliwa na Chunky Pandey na kumwambia atajitolea kuchukua nafasi ambayo Saif alikuwa amekataa.

download (1).jpeg
 
Back
Top Bottom