Mabilionea wanaochipukia kwa kasi Mbeya na Iringa

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
3,410
6,067
Achana na zile story za kina fresh ya Shamba,achana na story za wakinga na ushirikina,achana na hadithi za kina Jombi na mwenzake Mwamajuja,sana ni wazi kuwa Mbeya,Iringa na Njombe ndio Habari za town,tokea Iyunga hadi nzovwe,hadi mwanjelwa mbeya ni Boom,mwanzoni nilikua namfahamu Dandho tu,akiwa na malori zaidi ya mia tatu...na pale dandho complex tukienda kula raha...

mbeya imejengwa kwa kasi ya ajabu mno,kama Iringa na Makambako,hadi Njombe ndani ya Miaka
mitano mikoa kama Arusha na Moshi inaweza kuachwa kasi ya ajabu,lakini hii yote inatoakana na mwamko wa vijana wa mbeya,hasa Tunduma na Mwanjelwa.

tukisaidiana,napenda tufahamu kwa mikoa hiyo ni nani sasa wanakamata usukani,kwenye kila nyanja..

1.Dandho truck-Transportation and Leisure
2.Asas Dairy-Dairy Product
3.Sauli-Hotel and Cosmetics
4.....
5.....
6.....
 

4.Jacob Anyimike Aka Kasisi-Anamiliki Hotels kadhaa Mbeya na maduka ya Jumla
5.Tughimbe-Kumbi za starehe Mbeya na Truck kibao
 
Kuna haka kastaili kako ulikokuja nako ka Mabilionea sijui wababe wa miji gani...nasubiri umalize miji yote na mabilionea wako ukianza thread za mabilionea wa Imalinyi, Uporoto, Mdandu, Kinyangongwa na madibila unistue!
 
Kuna haka kastaili kako ulikokuja nako ka Mabilionea sijui wababe wa miji gani...nasubiri umalize miji yote na mabilionea wako ukianza thread za mabilionea wa Imalinyi, Uporoto, Mdandu, Kinyangongwa na madibila unistue!
mkuu unatokea igunga nn,huko nako nakuja usiogope kaka?
 
Hahaha huo utajiri mnaochukua kwa Mwakipande utawamaliza. Vijana wengi sana wa mikoa ya Mbeya na Iringa wanakufa na kuacha utajiri sababu ya ushirikina kwenye utajiri wao
 
Matajiri nyanda za juu wapo
1. Makambako
2. Njombe
3. Mbeya
4. Songea

Iringa mmm
 
Watajeni wote ili mabank na tra wasipate tabu kuwavumbua uko walipo jichimbia!

Baba nusa....mgahawa Iringa!
Nelkon....Kihesa mgahawa wa chai,wali na maandazi
Chuwa... mabanzi hevy,wali nyegere,na kibanda umiza!
Kisoma...chips mayai na mishikaki
 
Hahaha huo utajiri mnaochukua kwa Mwakipande utawamaliza. Vijana wengi sana wa mikoa ya Mbeya na Iringa wanakufa na kuacha utajiri sababu ya ushirikina kwenye utajiri wao
Huyo mwakipande ndio yule "ntaaramu" wa kutengeneza utajiri kupitia punje za mahindi zinazo donolewa na kuku?.

Nimeuliza kutokana na story ninazo zisikia kuhusiana na utajiri wa vijana wa kikinga toka makete.
 
Watajeni wote ili mabank na tra wasipate tabu kuwavumbua uko walipo jichimbia!

Baba nusa....mgahawa Iringa!
Nelkon....Kihesa mgahawa wa chai,wali na maandazi
Chuwa... mabanzi hevy,wali nyegere,na kibanda umiza!
Kisoma...chips mayai na mishikaki
!........umenichekesha sana na umenikumbusha mbali sana kwa Baba Chuwa!
 
Tatizo vijana wa nyanda za Juu Kusini na baba zao utajiri wao ni wa kishirikina,Yaani utajiri wa punje za mahindi kwa kumrushia kuku ndio umejaa sana Mikoa hiyo.

Kuanzia kwa Baba zao kina Mzalendo mpaka kina Nyagawa.Wamejaa mali za kishirikina tu,mambo gani mtu una pesa mabilioni halafu unashindia maandazi na mikate ya kikinga ya kwenye ganda la mgomba huku unashushia na juice cola,pakiti moja unatengeneza juice ndoo ya lita kumi.

Huu utajiri wa kununua kwa Mwandulami na kwa Mwakipande huu hauna maana,unakuta kijana ana hela kibao lkn analala kwenye ngozi,masharti ya kuoga Ijumaa tu saa sita usiku tena maji ndoo ya lika kumi.Vijana wana pesa lkn anaishi maisha ya kingese sana,hakuna cha bata wala nini..

Utajili upo kaskazini,kwanza wa kijanja...Kijana mdogo unakuta ana mkoko wa hatari,nyumba ya maana na maisha yanakwenda,lkn vijana wa kusini ana pesa kibao ila masharti ni kupanda fusso kila anaposafiri kufunga mzigo Dsm,unakuta kijana kuja Dsm Fastjet anaiogopa,yeye ni kuvizia fuso zinazoleta viazi vya chips Dsm anajifundika nyuma kama gunia la kiazi,njiani barid na mvua ni vyake

Wakati wa kurudi utamkuta Kimara Rombo anasubiria Fuso zilizoleta nyanya za Ilula na Kiazi cha Njombe ndio arudi nazo,mkononi ana kilambo cha maandazi na kopo la maji ya uhai kajaza juice za Sayona,sasa huu ndio utajiri au mateso??***** sitaki kabisa huu utajiri,mtu unakaa week bila kuchamba kisa mganga kakupa masharti ya kugusa maji Ijumaa tu katika week

Watoto wa Kusini utajili wao ni wa masharti sana,ndio maana kuna kipindi wakaanza kuchuna mpaka ngozi
 
Kwa anaejua maana halisi ya utajiri Iringa ndy kuna matajiri visiki toka miaka ya 80, hapo Iringa mjini na Mafinga watu pesa wanayo Mbeya wanasubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…