Serikali ichukue jukumu la ujenzi wa majengo ya biashara na makazi ili kuweka ufanisi mzuri kwenye mipango miji, miundombinu na kupendezesha muenekano wa mji kwa ujumlaUshauri wako au mapendekezo Yako ni yapi katika hilo.
Tunaomba utuoneshe picha ya Paa la nyumba yako
serikali ingechukua jukumu zima la ujenzi na raia wakawa wanachangia gharama nafuu kwa Kodi tungekua na miji mizuri sanaUsikute labda ni kwa sababu ya vimbunga na matetemeko ya ardhi, kwa hiyo ushauri wa makandarasi na wasanifu-majengo ni kwamba majengo almost yote yasivuke mita 20 kwenda juu.
Sifa hizi Serikali yako haina na haitakaa ije kuzimiliki.Serikali ichukue jukumu la ujenzi wa majengo ya biashara na makazi ili kuweka ufanisi mzuri kwenye mipango miji, miundombinu na kupendezesha muenekano wa mji kwa ujumla
Isiachie sekta binafsi na wananchi wa kawaida mambo yatakua hovyo sana ujenzi unaitaji umakini na uwezo wa hali ya juu sana
Tangu Tanzania ijulikane hakuna tetemeko Dar! Asante Mungu! Nyumba za chini zinaonyesha kiwango cha umasikini! Masikini wanaishi chini!Usikute labda ni kwa sababu ya vimbunga na matetemeko ya ardhi, kwa hiyo ushauri wa makandarasi na wasanifu-majengo ni kwamba majengo almost yote yasivuke mita 20 kwenda juu.
Kwa nini usigombee mwakani, mkuu?serikali ingechukua jukumu zima la ujenzi na raia wakawa wanachangia gharama nafuu kwa Kodi tungekua na miji mizuri sana
Serikali tayari ina mzigo mkubwa wa mambo mengi na imeshindwa kuyasimamia.Serikali ichukue jukumu la ujenzi wa majengo ya biashara na makazi ili kuweka ufanisi mzuri kwenye mipango miji, miundombinu na kupendezesha muenekano wa mji kwa ujumla
Isiachie sekta binafsi na wananchi wa kawaida mambo yatakua hovyo sana ujenzi unaitaji umakini na uwezo wa hali ya juu sana
Sure mkuu, serikali ipambane master plan ya mji na miundombinu iendane na ukuaji wa mji na kusimamia ubora wa ujenzi wa majengo ili kudhibiti ujenzi wa hivyo usiofuata viwangoSerikali tayari ina mzigo mkubwa wa mambo mengi na imeshindwa kuyasimamia.
Tanzania serikali inamiliki ardhi, kulikuwa hakuna haja shirika kama NHC kutokuwa na nyumba zake mpya standard za ghorofa 15 na zaidi maeneo ya mjini. Lakini NHC imeshindwa kujenga nyumba nafuu kwa wananchi wa kipato cha kawaida na cha chini. Hususan wafanyakazi wa taasisi za serikali. Ni kama vile baada ya kutaifisha nyumba za wahindi, NHC kwa kiasi kikubwa imeridhika.
Dar es salaam ni mji unaokua kwa kasi sana , karibu 5% annual growth. Maana yake katika miaka 15 ijayo, kwa kasi hii, idadi ya watu Dar ita double.
Bila kujenga juu tutapata tabu sana kui accommodate hii Dar nyingine ambayo tutaimeza ndani ya Dar ya sasa.
Serikali ina nafasi yake ya kujenga nyumba, lakini serikali haiwezi kujenga nyumba za kutosha. Kazi kubwa ya serikali ni kuweka standard, masterplan na kuhakikisha inafuatwa. Kuweka mazingira mazuri ya ukuaji wa uchumi watu wajenge vizuri.
Katika hili la masterplan tushaharibu sana. Mji haujafuata masterplan. Kila mtu kajenga kivyake, kila kitu kika sehemu.
Pia kuna changamoto kama za maji kupanda juu ghorofani. Miaka ya 80 Dar es salaam maji yalikuwa na presssure nzuri, kufikia niaka ya 90 kati, hapo Upanga tu ambapo sio mbali na mjini kati Mchafukoge ghorofa ya pili tu ilibidi mtu awe na pump yake kuvuta maji. Sijui kwa sasa hali ikoje.
Pia kuna huduma kama zimamoto, unapojenga maghorofa marefu ya ghorofa 15 na zaidi, kuna zimamoto za kutosha za kuweza kuzima moto ukiwaka juu huko?
Kuna changamoto nyingi, lakini hizi zote zinaweza kufanyiwa kazi kwa kuongeza vyanzo vya maji na kuboresha miundombinu ya maji kuzuia upoteaji wa maji.
Mji umekua sana lakini miundombinu haijaongezwa. Masuala kama zimamoto ni suala la kuongeza bajeti, kuongeza vitendea kazi na kuongeza mafunzo.
Kodi inalipwa, mji unaongezeka, walipa kodi wanaongezeka, hatuoni Fire Brigade nayo ikiongezeka.Kweli mji umekua sana tangu ulipokuwa unaishia Magomeni mpaka leo kituo cha Fire Brigade kimoja tu hicho hicho cha hapo Mwembetogwa Faya hatuna kingine?
Hapo kweli kujenga juu bila kujiongeza kwenye masuala ya uokoaji tutakuwa tunatengeneza tatizo tu.
Akionyesha pa lake niite jibwaUshauri wako au mapendekezo Yako ni yapi katika hilo.
Tunaomba utuoneshe picha ya Paa la nyumba yako