Mabasi ya mikoani kuwa na kituo kimoja cha kujisitiri

Revolution

JF-Expert Member
Feb 28, 2008
919
854
Habari Wandugu!

Leo kero yangu ipo kwa wasafirishaji wa abiria Mikoani haswa masafa marefu ya kuanzia masaa sita na kuendelea. Ni kawaida kwa wasafirishaji wa mabasi kutokuwa na vyoo ndani ya mabasi yao na pia kuweka sehemu moja katika safari nzima kwa ajili ya huduma za kijamii ikiwepo kula na kuchimba dawa. Pia wakifika hapo wanataka mtumie dakika kumi tu na hapa abiria wengi sana huwa wanaachwa.

Wadau kumbukeni abiria wenu mbalimbali wanapitia changamoto mbalimbali za kiafya. Abiria anatakiwa afurahie kusafiri na siyo iwe kero kwake. Abiria wengi wanahitaji kufika sehemu wanayokwenda na siyo wanataka kuwahi, hizo haraka zenu ni za nini??

Ushauri: Safari za kuanzia masaa tano na kuendelea ziwe na kituo kimoja hadi viwili vya abiria kushuka na kujihudumia katika mahitaji yao mbalimbali. Na kila kituo mtumie angalau dakika 20. Haraka ya nini ndugu zangu?

Kama hilo haliwezekani basi kituo kiwe kimoja ila mabasi yote yawe na vyoo ndani.

Ninaomba sana huu uzi uwafikie wanaumoja wanaomiliki mabasi Tanzania. Hata Shabiby na wengine wanaofanya biashara hii kisasa wameamua kuwaiga watoa huduma wa zamani ambao wanaendesha biashara kwa mazoea.

Nawasilisha
 
Nakumbuka Marekani na Canada Kuna huduma ya coaches ambapo mnakodi gari ambayo mpaka kuna jiko meza na vitanda vya kulala,safari sio utumwa ni experience
 
Dah! Usafiri wa umma kibongo bongo ni mateso sana. Mbaya zaidi kama una usafiri binafsi, na kwenyewe ni majanga tu uwapo barabarani. Maana siyo kwa kero zile kutoka kwa wale wapenda rushwa.
 
Back
Top Bottom