Mabadiliko ya Uongozi yaja CHADEMA: Lowassa Mwenyekiti, Mbowe Katibu Mkuu

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Taarifa mpya ninazowaletea leo ni kwamba CHADEMA wanapanga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020. Taarifa zilizovuja kutoka chanzo changu ndani ya Ufipa zinasema kuwa awali CHADEMA walikuwa na mpango wa kujaza tu nafasi zilizoachwa wazi na hasa nafasi ya Katibu Mkuu.

Hata hivyo, kutokana na kikao cha mashauriano ambacho kimefanyika juzi usiku nyumbani kwa Lowasa ambapo kimehudhuriwa na watu wazito wachache ndani ya CHADEMA kimeona kuwa kuna haja ya kufumua mfumo mzima wa uongozi ili kuweka watu ambao wanaamini kuwa watakivusha salama chama hicho katika kipindi cha kuelekea 2020. Watu wanaofikiriwa kujumuishwa kwenye safu ya uongozi ni wale waliomfuata Lowasa CHADEMA akiwemo Frederick Sumaye.

Chanzo changu ndani ya Ufipa ambacho hakijawahi kuniangusha kimenidokeza kuwa CHADEMA wana mpango wa kumchagua Edward Lowasa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho huku Freeman Mbowe anayeshikilia nafasi hiyo akiteuliwa kuwa Katibu Mkuu. Chanzo hicho kimesema kuwa maamuzi hayo ni kwa maslahi ya chama hasa ikizingatiwa uwezo na uzoefu wa Lowasa katika siasa za nchi hii.

Pia chanzo hicho kinasema kuwa muundo wa sasa haumpi Lowasa nafasi ya kufanya maamuzi ya chama na hivyo kuna haja ya kufumua mfumo mzima wa chama ili aweze kuwasimamia ipasavyo wabunge na madiwani waliochaguliwa kutokana na ushawishi wake. Chanzo hicho pia kimedokeza kuwa Lowasa anataka nafasi ya Uenyekiti ili aweze kusimamia ipasavyo Halmashauri walizoshinda UKAWA na hasa Ilala, Kinondoni, Mbeya na Jiji la Dar es Salaam ili ziongoze kwa ufanisi na hivyo zitumike kuwashawishi wananchi kumchagua mwanasiasa huyo katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Taarifa zinasema kuwa Freeman Mbowe kwa ushawishi wa Mzee Edwin Mtei ameridhia mabadiliko hayo na kukubali nafasi ya Katibu Mkuu wa chama na hivyo kufuta kauli ya Tundu Lissu kuwa viatu vya Dk Slaa ni vikubwa na hivyo hakuna wa kuvivaa ndani ya CHADEMA. Jopo hilo linaamini kuwa Mbowe ni mtu pekee anaweza kufuta historia ya Dr Slaa ya utendaji ndani ya CHADEMA.

Aidha, kwa vile Katibu Mkuu ni Mtendaji wa Chama, wanaamini kuwa Mbowe atasimamia ipasavyo mikakati yote ya chama hususan mkakati wa kukusanya fedha kutoka Halmashauri wanazoongoza ambazo zitatumika kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa 2020.

Jukumu langu ni kuwahabarisha tu.
 

Okay, umesikika.

Hela mbaya sana, yaani mtu anaandika chochote ili alipwe tu.
 
Asante mkuu. Hata hivyo sioni kwa nini Mbowe tu. Kwa maana nyingine aliyosema Sumaye ni sahihi , kwamba CHADEMA hakina wigo mpana wa uongozi. Pia ukweli kuwa chama kinaongozwa kutoka upande fulani wa nchi pekee. Hii inapaswa kutazamwa kwa jicho la tatu
 
Kila siku unakuja na mapya! Juzi ulituambia Tundu Lissu ndo atakuwa katibu mkuu leo umebadilisha gia hewani haya bana!
 
 
Juzi ulisema umepiga simu TCRA wakakwambia ile taarifa ya kufungia vyombo vya habari si yao lakini baadaye katika taarifa za habari ikabainika ni kweli,sasa kama unakosa vyanzo hiko katika taasisi za.serikali ya ccm za ukawa ndo utazipata?
 
Mkuu, nimekuletea taarifa ambazo ulikuwa huna. Wakati mwingine unafaa kuwa na shukrani
Tatizo sio taarifa tu ,ni uongo unaouleta kila siku humu ,mpaka sasa umekuwa mrithi wa shekhe yahaya ,umetabir sumaye kuwa katibu ,lisu kuwa katibu.....vyote hivyo umeleta hapa ,juzi ukaja na uzi lowasa ametengwa rasmi na chama.......ndo maana nasema wewe kwasasa ukisikia chadema pichu inakushuka yenyewe ,ila kumbuka tu kuwa mbowe ameoa hahitaji mke lowasa pia ameoa hahitaji mke .....na hata kama hawara wewe hufai una tabia za umbea na majungu sana dada liz.
 
Juzi ulisema umepiga simu TCRA wakakwambia ile taarifa ya kufungia vyombo vya habari si yao lakini baadaye katika taarifa za habari ikabainika ni kweli,sasa kama unakosa vyanzo hiko katika taasisi za.serikali ya ccm za ukawa ndo utazipata?
Haoni aibu na anasahau haraka balaaaaa
 
Yawezekana ila kwani kuna wakati walisema katibu atakuwa Sumaye lakini vijana CDM wali-react sasa kwa Mbowe watanywea.
 
Lowasa jana kanena na Mamya wapya wa kinondoni na Ilala tayari Lumumba imekua Nongwa.

Ni kwa miongo kadhaa CCM watachezeshwa makirkiri na Lowasa mpaka wakome.
CHADEMA kimejengwa kuzunguka watu. Sasa hivi kila kitu ni Lowassa tu, utadhani sio taasisi. Genge la wahuni haliwezi kujificha kamwe!
 
Juzi ulisema umepiga simu TCRA wakakwambia ile taarifa ya kufungia vyombo vya habari si yao lakini baadaye katika taarifa za habari ikabainika ni kweli,sasa kama unakosa vyanzo hiko katika taasisi za.serikali ya ccm za ukawa ndo utazipata?

Na mimi nilipiga simu TCRA wakasema hawajawafungia. Msikilize mtu wa TCRA mwenyewe akiongelea kutofungia hivyo vituo taarifa hii hapa acha kubeza watu wenye data.

 
Lowasa jana kanena na Mameya wapya wa kinondoni na Ilala tayari Lumumba imekua Nongwa.

Ni kwa miongo kadhaa CCM watachezeshwa makirkiri na Lowasa mpaka wakome.
Sasa nongwa ipo wapi? Kureveal mikakati yenu ndo nongwa? Kumbuka nimekuwa nikifanya hivi tangu muda mrefu. Jukumu langu ni kuwahabarisha akina Daudi Mchambuzi yale ambayo mnakuwa hamyajui
 
Hili nimeshalitolea ufafanuzi mara kadhaa. Kuwa huwa nawasilisha taarifa za wakati husika. Niliposema Jusa atakuwa Mgombea Mwenza wengi walipnga. Ila baadaye niliposema kuwa Juma Duni Haji ndiye Mgombea Mwenza pia walipinga mpaka ilipokuja kuwa revealled . Gia inapobadilishwa angani inabidi na wewe ubadili ya kwako humu JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…