the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 362
- 534
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limefanikiwa kudhibiti maandamano ya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA yaliyokuwa yamepangwa kufanyika siku ya leo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza hasa katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza DCP - Wilbrod Mutafugwa amesema maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika hayakuwa na uhalali wa kisheria hivyo Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza lilijipanga kuyadhibiti kwa kufanya doria maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza kuhakikisha hakuna vurugu ama maandamano yoyote yanayoweza kuleta uvunjivu wa Amani kwa wananchi ; na Jeshi la polisi halitasita kumchukulia mtu au kikundi cha watu hatua za kisheria watakaoandamana kinyume na sheria.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda amewataka wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA pamoja na wananchi kutii sheria na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama ili kufanikisha uchunguzi na upatikanaji wa mwanachama huyo anaedaiwa kupotea Februari 14 mwaka huu na kwamba serikali ipo macho kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwa salama.
Sanjali na viongozi hao, Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza Boniphace Nkobe, amewataka wanachama wa CHADEMA kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi na Serikali ili kuhakikisha mwanachama wao anapatikana akiwa salama.
Soma: Pre GE2025 - CHADEMA Mwanza kuandamana kesho Februari 19, 2025 hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupinga mauaji na utekaji wa viongozi wao
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025