Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,051
Nimeisikia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi, afande ACP Misime, ambayo alidai kuwa maandamano ya CHADEMAni ni haramu, Kwa hivyo wameyapiga marufuku.
Lakini katika taarifa hiyo ya Afande Misime, hajaongelea kabisa, madai ya CHADEMA waliyoyatoa katika taarifa yao ya kuitisha maadamano hayo.
Kwanza ni muhimu ikafahamika kuwa katika nchi inayoendeshwa Kwa njia ya kidemokrasia na Kwa mujibu wa Katiba yetu ya nchi, maadamano ya amani yanaruhusiwa na wajibu pekee wa Jeshi la Polisi ni kuyapa ulinzi Hadi mwisho wa maandamano hayo.
Pili, CHADEMA wamedai kuwa wanaipa serikali hii Hadi tarehe 21 mwezi huu, watoe taarifa ya walipo viongozi wao waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa hawajulikani na wakaendelea kueleza kuwa iwapo serikali hii haitakuwa imetoa majibu hayo ifikapo hiyo tarehe 21 mwezi huu, ndipo wao CHADEMA wataitisha maandamano hayo ifikapo tarehe 23 mwezi huu.
Niwakumbushe pia wajibu namba Moja wa Jeshi la Polisi nchini kwetu ni kuwalinda raia na Mali zao.
Soma Pia: Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu
Sasa niwaulize swali dogo tu Jeshi letu la Polisi, kama wajibu wenu namba Moja ni kuwalinda raia na Mali zao na Chama Cha CHADEMA kinadai kuwa Kuna viongozi wao wametekwa na hawajukikani walipo na ndiyo kinataka nyinyi Jeshi la Polisi muwaeleze wako wapi hao viongozi wao, hivi kosa la Chadema liko wapi hapo??
Jeshi i letu la Polisi, achaneni na utendaji kazi usiozingatia sheria zenu za PGO na Katiba ya nchi na badala yake, tekelezeni wajibu wenu Kwa weledi na Kwa kuzingatia Sheria za nchi hii
Mungu ibariki Tanzania