Maandamano ya CHADEMA: Jeshi La Polisi lathibitisha kukamata waandamanaji 14 ikiwemo viongozi wa CHADEMA

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
552
1,517
Jeshi la Polisi limetoa taarifa rasimi ya kuwakamata watu 14 ikiwemo baadhi ya Viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Lissu na Lema, ambapo wamedai kuwa viongozi hao wamekamatwa kufuatia mpango wa maandamano.

Wanawashikiria kwa sasa wanahojiwa kwa ajili ya hatua za kisheria.

Kamanda Muliro ametangaza kuwakamata viongozi mbalimbali wa CHADEMA ikiwemo Freeman Mbowe, Tundu Lissu pamoja na Godbless Lema.

Soma pia: LIVE Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024

Hawa jamaa wajaja sana,kukamatwa kwa leo ni kwa amani sana na hawawezi kufanywa chochote maaana ulimwengu umeona nani amewachukua..

Nilimuwa namsikia mbowe anasema kwamba hawa wamevaa uniform haina shida,hiyo ni baada ya kuulizwa na mwananchi kwamba hao polisi wanaokukatama hawajakuambia wapi wanakupeleka.

Mbowe bado ana imani na jeshi la polisi kuliko wafuasi wake..
 
Anayekumbuka maneno ya Lema kuhusu kupewa taarifa kwamba "jamaa" kafa hivyo yupo salama kurejea nyumbani kwa "mama"
 
Hao adhabu yao ni mahakamani halaf kila kesi ikitajwa zitolewe sababu za kuahirisha warudi rumande, wakili mtata wa serikali Wankyo Simon apewe kazi hiyo.

Tanzania is a sovereign country, nobody can force us what to do.

Asante sana IGP Wambura, Mdude Nyagali sijamuona kabisa leo
 
Mataahira kama wewe hamkutakiwa kuzaliwa Tanzania na nina wasiwasi wewe ni mhutu kama yule mwovu wa chato
 
Mnahangaika duniani kote kupata wahisani kuwapa misaada ya maendeleo, kila siku kiguu na njia.

Lakini kwa rasilimali hizohizo chache mnazitumia kwa mabilioni kugharamia jeshi la polisi kuendesha operesheni ya kuzuia maandamano ili tuu Waziri wa mambo ya ndani na IGP waliotakiwa kujiuzulu wasijiuzulu.

Hivi mnadhani wangejiuzulu na uchunguzi wa wazi ikiwa na kuwakamata na kuwahoji polisi wanaotajwa hayo maandamano yangeitishwa?

Mnatumia vibaya rasilimali za nchi kisha mkienda vijijini na kukuta shule hata Zahanati hazina vyoo eti mnashangaa!

Kwa mwanadamu mwenye maarifa KUPANGA NI KUCHAGUA, nyie mmekosa maarifa.
 
Mbowe amekamatwa na askari police tena wenye silaha nzito nzito wasiopungua 20 au zaidi. Hizi ni dalili za ushupavu au ulegevu wa jeshi letu?
Askari wetu n Waoga sana. Ukifika kituo cha police ucku wanakutreate kama Jambazi
 
Mitaa yenu ukiona kuna tukio la uhalifu au kuna sintofahamu fulani we piga sim au waite polisi
Sema cdm wako mtaani watakuja faster

Ova
 
Ni
Mbowe amekamatwa na askari police tena wenye silaha nzito nzito wasiopungua 20 au zaidi. Hizi ni dalili za ushupavu au ulegevu wa jeshi letu?
ushupavu kwani walitaka kuhakikisha kuna kuwa usalama eneo hilo na walitumia busara utadhani Polisi wa Ulaya, hawakudhalilisha yeyote aliyetii amri ya kukamatwa.
 
Mbowe amekamatwa na askari police tena wenye silaha nzito nzito wasiopungua 20 au zaidi. Hizi ni dalili za ushupavu au ulegevu wa jeshi letu?
IMG-20240923-WA0050.jpg
 
Mbowe amekamatwa na askari police tena wenye silaha nzito nzito wasiopungua 20 au zaidi. Hizi ni dalili za ushupavu au ulegevu wa jeshi letu?
Jeshi letu ni Shupavu mnooo. Wananchi wa Tanzania waliendelea na harakati zao za kimaisha kama kawaida. Hawakuwa na habari kabisa kuhusu maandamano.

Hongera sana kwa Jeshi letu Polisi na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama.
 
Polisi hawabebi chaki, sio walimu. Wanabeba bunduki.

Mbowe hakuwa peke yake, alikuwa na supporters wake ko tarajia lolote ndo maana they come well prepared coz they had expected the unexpected
 
Kama ni waoga mbona uliwaogopa na haukuandamana? KUMBAVU!!!
Maboya tu yale, kama wao ni miamba si wangeacha silaha na makorokoro mengine wakaenda kumkamata wakiwa mikono mitupu?
Kwa akili yako, nani boya kati ya wanaume zaidi ya 20 pamoja na silaha kwenda kumkamata mwanaume mmoja asiye na silaha.
 
Back
Top Bottom