𝐌aandamano ni Haki Kikatiba na msingi muhimu kwenye nchi yenye Demokrasia. Waandamaji wapewe ulinzi

Sking zone

Member
Jun 20, 2024
12
7
Ni haki na inahitajika wapewe ulinzi wa hakika, kwani ni moja ya misingi kidemokrasia, maandamano hahajafanyika hivyo uovu wa maandamano haujaonekana.

Watakapofanya maandamano yao kwa kusababisha vurugu, hapo sheria ndipo ifate mkondo wake lakini pindi maandamano bado hata kufanyika sheria iwalinde hao na waandamanaji wapewe ulinzi.

𝐀𝐔 πŒππ€π’π„πŒπ€π‰π„ 𝐍𝐈𝐍𝐘𝐈 π–π€ππ€π‰π€πŒπˆπˆπ…πŽπ‘π”πŒ?

Pia soma
- News Alert: - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

- Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea
 
Wapate mkong'oto kwanza halafu ndo sheria inafuatia baada ya hapo. Mzee wa hekima mbowe alituasa kuwa sumu haionjwi kwa ulimi.
Wewe acha mawazo ya uchawa!

Nani alikwambia kuwa eti Chadema, wamepanga maandamano, Kwa nia ya kuleta vurugu??

Kwanza lazima utambue kuwa wajibu wa Jeshi la Polisi namba Moja ni kulinda uhai wa raia na Mali zao.

Madai ya Chadema, yapo wazi kabisa, wameipa serikali hii, ifikapo tarehe 21 mwezi huu, hao akina Soka ambao wametekwa na watu wasiojulikana, iwapo bado watakuwa hawajukikani wako wapi, ndipo wao Chadema, wataitisha maandamano yao ifikapo tarehe 23 mwezi huu.

Maandamano hayo ni halali Kwa mujibu wa Katiba yetu, sasa hao Polisi, wanaopiga marufuku maandamano hayo, ndiyo wanajaribu kuivunja Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania!😳
 
Watakapofanya maandamano yao kwa kusababisha vurugu, hapo sheria ndipo ifate mkondo wake lakini pindi maandamano bado hata kufanyika sheria iwalinde hao na waandamanaji wapewe ulinzi.

𝐀𝐔 πŒππ€π’π„πŒπ€π‰π„ 𝐍𝐈𝐍𝐘𝐈 π–π€ππ€π‰π€πŒπˆπˆπ…πŽπ‘π”πŒ?
Ushauri wangu Ushauri kwa CHADEMA: Japo ni Haki, lakini chondechonde Msiandamane. Mwenye Nguvu Mpishe!
P
 
Nilitegemea ile barua ya polisi iwe inashauri kufuata taratibu na sheria juu ya maandamano.

Au wao wanapenda jina lao litumike kwenye kashfa ilihali sio wao? Kama ww sio mtekaji kwanini uzuie maandamano ya kupinga utekaji?
 
Ni haki na inahitajika wapewe ulinzi wa hakika, kwani ni moja ya misingi kidemokrasia, maandamano hahajafanyika hivyo uovu wa maandamano haujaonekana.

Watakapofanya maandamano yao kwa kusababisha vurugu, hapo sheria ndipo ifate mkondo wake lakini pindi maandamano bado hata kufanyika sheria iwalinde hao na waandamanaji wapewe ulinzi.

𝐀𝐔 πŒππ€π’π„πŒπ€π‰π„ 𝐍𝐈𝐍𝐘𝐈 π–π€ππ€π‰π€πŒπˆπˆπ…πŽπ‘π”πŒ?

Pia soma
- News Alert: - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

- Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea
Haki zote za kikatiba na zisizo za kikatiba zina masharti yake na mazingira yake. Maandamano ni haki yenye mipaka yake, siyo kila maandamano yataruhusiwa. Soma sheria

Sheria inakitaka chama cha siasa kutoa taarifa angalau saa 48 kabla ya siku ya maandamano hii ni kwa mujibu wa K/F 43 (1)cha CAP 322. Kifungu 43(2) kinaruhusu kuendelea na maandalizi ya maandamano hadi utakapopata zuio la maandamano. Lakini kifungu cha 43(3) kinampa mamlaka Polisi ofisa aliyepelekewa taarifa, akifanya tathmini kuwa maandamano yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani, atajibu barua kukataza maandalizi na ufanyikaji wa maandamano.

Sasa akili ya kawaida tu, Rais ameyakataa na kuahidi taarifa, IGP amekataa na kusema yanaashiria uvunjifu wa amani kumbuka kuna kauli mbiu SAMIA MUST GO, mkuu gani wa Polisi wilaya atajichanganya kutoa baraka ya maandamano kufanyika?

K/F cha 43(6) kinamtaka mtu aliyeitisha mkutano iwapo ataona katazo la polisi hakulipenda, akate rufaa kwa waziri. Sasa CHADEMA wanataka SAMIA aondoke, MASAUNI aondoke na WAMBURA aondoke, sasa nani atakubali maandamano hayo? si kujitafutia matatizo?
 
Back
Top Bottom