Maandalizi ya kuelekea Kijijini!

sirjohn

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
767
677
Salam mkubwa!


Nataka kwenda kuishi kijijini, ni kijiji gani kizuri hapa tz mkoa wowote ambao ntapata huduma zote za kibinadamu/kijamii mfano!

hospitali
shule kwa ajili ya wanangu
mashamba kwa ajili ya kilimo
barabara nzuri
usalama kama vile polisi
maduka kwa ajili ya mahitaji ya kila siku
kumbi za starehe kama vile club za pombe hasa za kienyeji, hotel kwa ajili ya wageni watakaonitembelea..



Nataka pia nikagombee wenyekiti wa kijiji.
 
Unapaswa ukazindikwe kwanza kwa mganga uwe fit, vinginevyo utapigwa kipapai.
 

Kama uko serious, vijiji vya Msowelo, Mvumi na Rudewa katika wilaya ya kilosa vitakufaa sana.
Barabara nzuri ya lami kutoka Dumila
Maduka yapo na pamechangamka
Starehe utafanyia bar zenye kumbi
Wageni watapata guest nzuri sana ya kisasa Msowelo
Panafikika kirahisi na vyombo vya usalama
Mashamba mazuri na vyanzo vya maji kama mito Msowelo na Wami (Maji mwaka mzima)
Shule za kiwango cha vijiji vya wastani Tanzania
 

naomba tuwasiliane inbox..ntakuPM. niko serious na kwa maelezo yako kama ni kweli hicho kijiji kinafaa japo ngoja tusubri wengine watasema wapi pazuri zaidi.
 
sasa maeneo ya pale sekei ni sawa si niko arusha mjini ..nataka kijijini kabisa
Kumbe we ni hutaki hata kuona magari hahaha basi nenda Ng'iresi hahahah huko magari utakayo yaona ni ya wazungu wakienda water falls basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…