Good morning....
Wewe ma mwenzi wako mmegombana, ila mkosaji ni wewe hapo assume umefumwa na mawasiliano ya mchepuko, mwenzio anaamua kukuuliza/kukuambia kistaarabu kabisa tena kwa sweet language "mpenzi ni hivi ni hivi nimesikia, nimeona unatembea na fulani......
Wewe mkosaji sasa uvimbe, unune, uje juu, kijasho kikutoke yani unafura kama nyoka ilhali umekosea na ni kweli umekosea. Muda huo mwenzio hata hana hasira na wewe anakusemesha vizuri mkosaji umevimba vishavu kama viandazi yani unataka hadi uombwe msamaha.
Maana yake huwa ni nini jamani? Kuelewa akili za binadamu ni ngumu, Make hii ni zaidi ya defensive mechanism
. Unakua hutaki kuulizwa? Sasa hii inawezekana vipi ukose usiulizwe? Afu mbona kama kuulizwa inaleta unafuu flani kuliko kunyamaziwa?
. Unataka kuombwa msamaha? Kwa kipi sasa ulichokosewa?
Hakika huu ni ujinga first class japo maana yake huwa siijui, nishaiona mara nyingi.
Nb : 1:kufumwa ni mfano tu, chukulia kosa lolote lile ilmradi kosa
2: hii inahusu jinsia zote mwanaume na mwanamke