Maajabu ya mtu mwenye sura tatu

chase amante

JF-Expert Member
Feb 24, 2018
5,616
2,126
Habari wakuu,

Kwenye maisha Kuna mambo mengi na mengi bado hayafamiki,lakini Kuna msemo wa wahenga kua ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni.

Mimi ni kijana mwanaume ambayo katika pitapita zangu nimeona mambo mengi lakini Kuna hili moja limenitatiza.

Kipindi nipo chuo mwaka 2018 nilishawahi kukutana na Binti dar es salaam katika chuo X.kiukweli nilivutiwa na yule Binti kwani nilikuwa nikisoma naye darasa moja.

Lakini,nilivyokua nikimchunguza nilikuja ona jambo la ajabu kidogo.Jambo lenyewe ni kua yule Binti alikua na sura tatu.

Sura ya kwanza ilkua ni ya mwnafunzi mpole na mkarimu aliyejibidiisha darasani.

Sura yake ya pili ni Binti aliekua msiri na mwenye kupenda kuchunguza mambo na kujihusisha na umalaya.
Sura ya Tatu ni ya Binti mwenye uwezo wa kuwepo kila mahala nilipojaribu kumkwepa.Yaani,kila eneo nililodhani nipo mbali na yeye na hawezi kulijua,basi yeye alikua anakuwepo eneo hilo bila mimi kufahamu kua yupo.

Hizi sura tatu nilizijua baadae sana baada ya kumchunguza sana na ilkua baada ya kumaliza chuo ndipo niligundua jambo hili.binti alikua na maarifa mengi ya kubadili tabia kulingana na eneo,kutambua saikolojia ya mtu na anachowaza na mwisho kabisa ni uwezo wake mkubwa wa kushawishi na kuwatega WANAUME wengi wamtongoze.

Jambo hili lilinifanya nijiulize kua je,huyu Binti ni Malaya mzoefu? Au ni jini? Au ni mpelelezi wa Siri aliyetaka kujua taarifa za wanafunzi wengi?.katika kuwaza kote sikulipata jibu.

Narudisha kwenu wakongwe huu mpira .hivi huyu Binti alikua na lengo gani au alikua na mission ipi pale chuo? Na je ,hizi sura zake tatu tofauti zilikua na maana ipi?
 
Back
Top Bottom